Kocha Pablo apewe Simba kwa muda mrefu

Kocha Pablo apewe Simba kwa muda mrefu

Huja

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2021
Posts
1,167
Reaction score
1,848
Hii ni kwa viongozi wa SIMBA. Nimeangalia style ya simba nimegundua kuwa PABLO ni kocha mzuri.

Aliikuta wachezaji wakicheza individual na sio team work. Taratibu naona simba wanavyocheza pasi na soka la haraka.

Simba hapo ilipo inahitaji tu aina fulani wa wachezaji then aweze kuwaunganisha, naamini simba inaweza kutisha AFRICA.

Tumpe muda wa kutosha PABLO. Shiida ya soka la Tanzania washabiki wamejaa kukosoa na pressure nyingi bila kuangalia mambo ya kiufundi. Najua kuna watu wanaokosoa namna anavyopanga na kufanya rotation ya kikosi lakini bado naamini kuna kitu cha kiufundi katika brain yake.

Simba inahitaji kujenga falsafa yake, kwa kuziangalia pia timu zenye mafanikio kama Mamelod Sundown, TP Mazembe, Al Ahly n.k na kuachana na mazoea ya ajiri - fukuza.

Bila ya hata kujali mwenendo wa msimu huu, ila kama simba inataka maendeleo ya muda mrefu, hasa kimaitaifa basi tumpe muda na support PABLO.

Sent from my CPH1933 using JamiiForums mobile app
 
Ila amefeli kuwaelekeza wachezaji wake kuhusu kukosa kosa magoli ya wazi. Hilo ni donda ndugu kwa Simba. Wannatengeneza nafasi sana lakini wanachemka kwenye umaliziaji
 
Tatizo sio pressure tatizo ushindani kwenye manunuzi yakocha watukati hufaidika nalo huyu kocha watuachie hata misimu tano ijayo
 
Malengo ya Simba iwe kwenye kujenga timu upya na kufanya vizuri CAF. Mwakani target iwe kushiriki CAF na ubingwa wa Tanzania.
 
Ila amefeli kuwaelekeza wachezaji wake kuhusu kukosa kosa magoli ya wazi. Hilo ni donda ndugu kwa Simba. Wannatengeneza nafasi sana lakini wanachemka kwenye umaliziaji
Kabsa aseee na kuwaruhusu kupack bus aseeeee
 
Pass za nyuma zikizidi sana pia zina-bore
 
bado hajaridhika na wachezaji wengi hata juzi kwenye post match press alisema nafikiri anasubiri kwa hamu usajili mpya
 
Ila amefeli kuwaelekeza wachezaji wake kuhusu kukosa kosa magoli ya wazi. Hilo ni donda ndugu kwa Simba. Wannatengeneza nafasi sana lakini wanachemka kwenye umaliziaji
Ilo sio jukumu la kocha ni jukumu la mchezaj
 
Back
Top Bottom