Kocha Taifa Stars ajuta kuwaacha Kapombe, Shabalala

Kocha Taifa Stars ajuta kuwaacha Kapombe, Shabalala

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
KOCHA TIMU YA TAIFA, ANAWAULIZA NINI?
1. Kocha timu ya taifa, anawauliza nini?
Si wa timu ya taifa, anawaambia nini?
Vipi hamko Taifa, au kwamba kuna nini?
Mpira wa Tanzania, tunaujua wenyewe.

2. Hao wachezaji bora, wengine hawafanani,
Kwenye namba zao bora, wakiwapo uwanjani,
Kuwa Taifa hasara, kocha anasema nini?
Mpira wa Tanzania, tunaujua wenyewe.

3. Tulishangaashangaa, wameachwa ni kwa nini?
Tulikatishwa tamaa, kocha anafanya nini?
Ndo maana twashangaa, anawauliza nini?
Mpira wa Tanzania, tunaujua wenyewe.

4. Wamekipiga vijana, kwani nani hawaoni?
Goli wamelinda sana, wa kuwapita ni nani?
Wameovalepu sana, kocha sasa ana nini?
Mpira wa Tanzania, tunaujua wenyewe.

5. Kweli kocha ni mgeni, aloichagua nani?
Aliwaacha kwanini, ndiyo maswali kichwani,
Jibu anajua nani, hebu alete mezani,
Mpira wa Tanzania, tunaujua wenyewe.

6. Kapombe leo kacheza, kocha ameona nini?
Na Hussein amecheza, wamemuonesha nini?
Ni nini awauliza, jibu atatupa nani?
Mpira wa Tanzania, tunaujua wenyewe.

7. Heri tunawatakia, na uchezaji makini,
Wale waliwasagia, aibu hadi moyoni,
Hawa ni Watanzania, hawako huko kwanini?
Mpira wa Tanzania, tunaujua wenyewe.

8. Pamoja picha za Simba, ushindi mamilioni,
Picha nyingine yatamba, kocha anasema nini?
Maswali tazidi imba, hao waliachwa nini?
Mpira wa Tanzania, tunaujua wenyewe.
 
Back
Top Bottom