Kocha wa Arsenal alikuwa kocha wa Weah, amesema hakuwahi kufikiria mchezaji huyo angekuwa Rais

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827



George Opong Weah akiwa na Ronaldo


Hapa akiwa na KOCHA MARIDADI Mzee Wenga ANAKUFUNDISHA MPAKA KUWA RAIS WA NCHI😱😱😱😱

Raia wa Liberia wanasubiria kwa hamu tukio hilo la kuapishwa kwa Rais wao George Opong Weah,ambapo wamekesha katika uwanja wa mpira wa taifa,mahala ambapo leo historia ya mwanasoka huyo inajiandika upya kutoka kung'ara katika soka na hatimaye kuingia katika uga wa siasa kuwa rais wa taifa hilo lenye historia ya milima na mabonde kisiasa.

Aliyewahi kuwa meneja wa George Weah katika klabu ya Monaco inayocheza ligi kuu ya Ufaransa Arsernal Wenga amealikwa na atakuwepo katika uapisho huo.

Meneja huyo wa Arsenal alikuwa meneja wa Weah katika klabu ya Monaco inayocheza Ligi Kuu ya Ufaransa miaka ya 1990 na amesema hakuwahi kufikiria kwamba wakati mmoja mchezaji huyo angekuwa rais.

George Weah, maisha yake ya utoto,yalikuwa katika mazingira duni katika mji mkuuwa Liberia Liberia Monrovia, alipata mafanikio makubwa katika medali ya soka na kufanikiwa kuchezea timu kadhaa barani Ulaya ikiwemo Chelsea na AC milan.

Ni Muafrika pekee kuwahi kushinda tuzo mchezaji bora wa FIFA na tuzo ya Ballon.

Weah aliingia katika siasa baada ya kustaafu soka mwaka 2002 na akawa miongoni mwa maseneter katika bunge la Liberia.

Aligombea urais mwaka 2005 ,na Alimshinda Bi Johnson Sirleaf wakati wa duru ya kwanza katika uchaguzi huo lakini kashindwa katika duru ya pili ambapo kambi yake ilisusia kushiriki katika duru ya pili.
 
Mungu anapanga mambo yake kimya kimya kwa hiyo haikuwa rahisi kwa Wenger kuhisi kuwa weah atakuja kuwa raisi wa Liberia
 
Namshauri Wear amuige Wenger asikubali kuachia madaraka kirahisi rahisi
 
Wenger alivyosema hivyo,je kuna mchezaji yoyote yule ambae huyo aliwaza anaweza kuwa Rais na akawa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…