Haya maswali wanayouliza waandishi wa habari wa kitanzania hakika nimeamini wao "Ndio wanaochafua nchi yetu huko nje"" na si mara ya kwanza hata kocha wa Simba wa sasa amekuwa akilalamika kwa maswali ya kijinga saana wanayouliza waandishi wetu wa habari achilia mbali "broken english" najua huo ni ugonjwa wa Taifa kuanzia "Magogoni" lakini angalau basi hata " thamani" ya swali lenyewe basi liwe la maana ...ninaomba kama Simba ikishinda kesho kwenda hatua ya robo fainali katika "press conference" zijazo kama wahariri hawawezi kwenda wao basi wawape kazi hiyo wakina Paschal Mayala au Dr.leakey kujaribu kutuondolea aibu hii ya kuchafua taswira ya nchi... Na hii sio kwa michezo tu hata pale wanapokuwa wanawahoji watu muhimu kama viongozi wakubwa wa kisiasa!