Kocha wa AS Vita akizungumza na Waandishi wa habari kuelekea pambo la klabu yake dhidi ya Simba uwanja wa Taifa

kasenene

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2008
Posts
1,632
Reaction score
2,413
Haya maswali wanayouliza waandishi wa habari wa kitanzania hakika nimeamini wao "Ndio wanaochafua nchi yetu huko nje"" na si mara ya kwanza hata kocha wa Simba wa sasa amekuwa akilalamika kwa maswali ya kijinga saana wanayouliza waandishi wetu wa habari achilia mbali "broken english" najua huo ni ugonjwa wa Taifa kuanzia "Magogoni" lakini angalau basi hata " thamani" ya swali lenyewe basi liwe la maana ...ninaomba kama Simba ikishinda kesho kwenda hatua ya robo fainali katika "press conference" zijazo kama wahariri hawawezi kwenda wao basi wawape kazi hiyo wakina Paschal Mayala au Dr.leakey kujaribu kutuondolea aibu hii ya kuchafua taswira ya nchi... Na hii sio kwa michezo tu hata pale wanapokuwa wanawahoji watu muhimu kama viongozi wakubwa wa kisiasa!

 
Angalia tu microphones brand utajua walijaa waandishi wa aina gani. Kweli hizi online tv zimetoa ajira nyingi lakini kuwepo na udhibiti kidogo kwenye elimu. Kinge ni tatizo kwetu wengi lakini hii sasa ni aibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Walipoamua ni English na French,kuna mmoja akasema Duh,ila angewarahisishia wanauliza kwa kiswahili then anatafasiri kwa english kama inavyofanyanywa mechi za champions ligue Ulaya.
 
Hii lugha hii kuna mtu katuloga sehemu!!! yaani unaona waandishi wa habari wanaogopa kabisa na wale wanaojitutumua wanauliza maswali ya mkato kama wanafanya mtihani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…