Kocha wa Bandari FC Mwalala: Ningecheza na Yanga SC nisingepata nilichokitaka ila Simba SC wamenifundisha Mpira wako vizuri

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Mnapoambiwa kuwa Simba Sports Club ni Timu Kubwa Barani Afrika msiwe mnabisha ili mradi tu mbishe. Kocha wa Bandari FC ambaye aliwahi kuwa Mchezaji Mwandamizi na Tegemeo kabisa hada kwa upande wa Ushambuliaji wa Yanga SC Ben Mwalala amemaliza kila Kitu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari tena bila hata ya ' Unafiki ' au Upendeleo wowote alisema kuwa mara baada ya Mechi yake na Simba SC Viongozi wa Yanga SC walimfuata Kumuomba aibakishe Timu yake ili wacheze nao lakini hakuwachelewesha kuwajibu ambapo aliwaambia kuwa kwa Yanga SC ilivyo sasa isingempa ' Changamoto ' ambazo alikuwa akizitaka ili Kuijenga vyema Timu yake ila alipocheza na Simba SC japo alifungwa lakini pia alifurahi na kuwashukuru Simba SC kwani walimfundisha Mpira na pia walimsaidia Kuonyesha Mapungufu ya Timu yake na akasema kuwa kama kuna Timu ambayo Kwanza imepata Kocha Mtaalam kabisa na imesajili ' Kitaalam ' kabisa kwa Ukanda huu wa Afrika Mashariki basi ni Simba Sports Club.

Namalizia tu kwa kusema Pyramid FC hata umpeleke Mwanza au Zanzibar ( Gombani Pemba / Amaan Unguja ) au umbakishe hapa hapa Dar es Salaam ila ' Kipigo ' chake kipo pale pale. Ushindi wako kwa Pyramid FC hapa Nyumbani ni Sare ( Draw ) tu na hata ukibahatisha Kumfunga basi iwe isiwe ni lazima tu na Yeye atakufunga angalau Goli moja hapa ili ' akakuue ' vizuri Kwake Misri. Kudadadeki!

Akhsante sana na mno Kocha wa Bandari FC ' Mtaalam ' Ben Mwalala kwa kusema ukweli wako juu ya Simba Sports Club.
 
Duh! Mkuu unajua kutabiri, yaani matokeo yote yanayo patikana katika mchezo wa mpira wa miguu umeyaweka.
Hongera sana.
 
kuna Popoma anajiita An Eagle anasema Vyura lazma washinde game na Waijipti
 
Wilka katika miaka mitano na nusu kacheza game 35 na kufunga magoli 6,Tz ndiyo ligi mkuu yake ya kwanza kucheza,maana alikuwa anacheza mabonanza tu huko,sasa we mbumbumbu badala ya kuhangaika na mabingwa wa kihistoria wa Tz pambana na viongozi wako waliokuletea vimeo,haiwezekani mchezaji professional league kaanza kucheza 2016 wakati ana 25+.

Tatua kwanza shida zako nyumbani kwako,ndiyo uje nje
 
Inawezekana Mwalala ameongea ukweli, ila Yanga itabaki kuwa ni Timu ambayo haijatolewa round ya awali na inakaribia kutinga Group stage. Hata ikiishia hapo walau kuna kitu cha ziada imekionyesha kuliko KMC na Timu zingine.
 
Hivi profile la Molinga linasemaje mana hata Google hawamjui?
 
Hivi profile la Molinga linasemaje mana hata Google hawamjui?
Hajacheza zaidi ya miezi 6,sasa nawewe leta hizo za wabrazil uone tofauti na Molinga aliyekuwa anacheza official first league
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…