Kocha wa kenya arudishwa nyumbani kwa kudanganya vipimo vya mkojo

Kocha wa kenya arudishwa nyumbani kwa kudanganya vipimo vya mkojo

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
15,692
Reaction score
23,038
Kocha wa riadha wa Kenya wa mbio fupi za mita 800, John Anzrah amerudihwa nyumbani Kenya kutoka kwenye michezo ya Olimpiki nchini Brazil kwa makosa ya udanganyifu.

Bwana Anzrah aligundulika alikuwa akitumia taarifa za mwanariadha wake aitwae Ferguson Rotic kwa kutoa vipimo vya mkojo vya kwake badala ya vile vya mwanariadha huyo.

Na ili kuweka rekodi mbaya kabisa bwana Anzrah akasaini fomu za kufanyiwa majaribio hayo ilhali akifahamu kuwa yeye hakuwa Gerguson Rotic.

Rotic anatarajiwa kukimbia mbio hizo leo Ijumaa na aliwahi kushiriki mashindano hayo mwaka jana mjini Beijing na kushika nafasi ya nne.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba Rotic alimwazima kocha wake kadi yake ya kuingilia kwenye milango mbalimbali ili aitumie kwenda kunywa chai ya asubuhi kwenye moja ya migahawa iliyopo kwenye kijiji cha michezo.

Lakini alipokuwa akirudi kwenye kambi ya timu ya Kenya alikutana na ofisa anaechukua sampuli ya mkojo ambae alikuwa akimtafuta Rotic ambapo meneja wake aliamua kutoa sampuli ya mkojo wake badala ya sampuli ya Rotic.

Ferguson Rotic baadae alikuwaj kutoa sampuli ya mkojo wake ambapo ulipopimwa ulionekana uko safi na ule wa Anzrah nao haukukutwa na tatizo ila kukawa na sampuli mbili tofauti.

Kamati ya kimataifa ya Olimpiki tayari imeanza taratibu za kinidhamu na Anzrah amerudi Nairobi akiwa ni ofisa wa pili baada ya ofisa mwingine bwana Michael Rotich ambae aliandaa utaratibu wa kulipwa pauni za Uingereza 10,000 kwa kutoa taarifa za tahadhali kuhusu ni muda gani vipimo vitakuwa vinachukuliwa.

Waafrika ndivyo tulivyo.

NB: Habari hii imeenea vyanzo mbalimbali vya habari duniani na ni aibu sana.
 
....swali la msingi; kwanini alifanya hivyo km vipimo vyote vinaonesha viko safi?!, huyu jamaa hakuwa na nia mbaya, kiukweli naweza kumtetea popote!, japo ni kweli kuna udanganyifu, ila kwasababu lengo kuu la kuchukua vipimo ni kupima km mtu anatumia madawa ya kuongeza nguvu, na hiyo sample imekutwa salama, sioni sababu ya kuwapa adhabu kubwa sn.

...ila wakenya nao wanahukumiwa kwa matendo yao, wanariadha wengi wa kenya wamekutwa na hatia kwenye hii issue ya kutumia madawa yaliyopigwa marufuku michezoni, they set very bad precedence!
 
Back
Top Bottom