Kocha wa KMC Mburundi Thierry Hitimana apimwe Akili upesi huenda hayuko sawa

Kocha wa KMC Mburundi Thierry Hitimana apimwe Akili upesi huenda hayuko sawa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kwenye Mchezo wa Jana ( Wenyeji wa Mechi ) walikuwa ni KMC ambao kwa sababu zao wenyewe waliamua Kuukimbia Uwanja wao wa Nyumbani wa Uhuru Mkoani Dar es Salaam na kuamua kuipeleka Mechi hii CCM Kirumba Mkoani Mwanza.

Baada ya Utangulizi huu sasa GENTAMYCINE nawawekeeni Nukuu ya Kauli ya Kocha wa KMC baada ya Kufungwa na Simba SC jana CCM Kirumba.....

"Wenzetu ( Wapinzani wetu Simba SC ) wao walitangulia Siku nyingi tu kuwepo hapa ila Sisi tumetoka mbali na bado tuna Uchovu wa Safari pamoja na Ratiba ngumu ya Ligi Kuu"

Popote pale mlipo Madaktari wa Magonjwa ya Akili ikiwapendeza anzeni pia kufanya Ukaguzi wa Wagojwa wenu kwani huenda hata huku katika Soka la Tanzania ( Bongo ) hasa hii NBC Premier League kukawa na Wateja wenu wengi kwa upande wa Makocha.
 
Walifuata mapato na hilo limefanikiwa, yaliyobaki ni ngonjera za mfamaji
 
Kwani alieamua wakachezee Mwanza ni Hitimana? Hapo anafikisha ujumbe Kwa viongozi wake walioamua hivyo na kuchelewesha timu kusafiri.
Kupitia haya maelezo yako hapa, mimi Tate Mkuu, nikiwa na akili zangu timamu! Napendekeza mtoa mada ndiyo akapimwe akili!

Imagine ameshindwa kabisa kugundua akili kubwa ya huyo kocha wa KMC. Hayo maneno ni ujumbe tosha kwa wamiliki wa KMC kwa kitendo chao cha kuipeleka hiyo mechi Mwanza, bila ya sababu za msingi! Na mwisho wa siku wakaishia tu kuwachosha wachezaji.
 
Back
Top Bottom