Kocha wa RB Leipzig kurithi mikoba ya Flick

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
NAGELSMANN KURITHI MIKOBA YA FLICK

Taarifa ambazo zimeripotiwa na vyombo mbalimbali vya Habari toka Nchini Ujerumani na hata Ulaya kwa Ujumla ni kuwa klabu ya Bayern Munich inamtazamia Kocha wa RB leipzig Julian Nagelsmann kuwa ndiye mrithi wa mikoba ya Kocha Hans Flick ambaye anatarajia Kuachana na Klabu hiyo mwishoni mwa msimu.

Kumbuka kuwa miaka kadhaa nyuma kocha huyo alieleza nia yake ya kuja kuifundisha Bayern Munich akiwa anahudumu kwenye klabu ya TSG Hoffenheim ,pia wiki Moja imepita tangu aseme kuwa hana mpango wa kujiunga na miamba hiyo.

Vyanzo kadhaa vimeeleza kuwa Nagelsmann ameiomba klabu yake ya RB Leipzig awaze kusitisha mkataba wa kukinoa kikosi hicho ili kutimiza ndoto yake ya kuifundisha Bayern Munich.

[emoji3578][emoji3578][emoji3578][emoji3578][emoji3578]Maoni yangu[emoji3578][emoji3578][emoji3578]
------------------------------------------------------------------
Nagelsmann ni miongoni mwa makocha vijana ambao wanafanya vyema kwenye soka la Ujerumani lakini hata Ulaya kwa ujumla kwa sasa akiwa na miaka 33.

Kafanya vyema akiwa na klabu ya Hoffenheim ambapo alifanikiwa kuwaokoa wasishuke daraja lakini pia walimaliza nafasi 4 za juu kwenye Bundesliga ndani ya msimu wa 2016/2017.

Huku msimu uliyopita akiishia hatua ya nusu fainali kwenye Mashindano ya UCL akiipoteza mbele ya Miamba ya Ufaransa PSG.

Nagelsmann ni muumini wa soka la kushambulia lakini hata hivyo anatajwa kuwa kocha anayemkubali zaidi ni Jose Mourinho.

Ninaamini kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kocha huyo kutua Bayern Munich ana akawa na msaada mkubwa kwenye kikosi hicho na taifa la Ujerumani kwa kiasi kikubwa.

1.Umri wake unawapa faida zaidi kikosi Cha Bayern Munich kuwa na mipango naye ya muda Mrefu kwani ni mzawa ambaye pia alihusishwa kwa muda Mrefu kujiunga na Bavarians.

2.Bavarians katika kipindi ambacho wanahitaji kujenga timu yao ni sasa na Nagelsmann ni kocha mzuri katika kujenga timu anaweza kufanikisha adhama hii ndani ya Bayern Munich ambao kwa kiasi kikubwa huamua ubora wa kikosi Cha Timu yao ya Taifa.

Mchana mwema wapenda soka wote na poleni wananchi wenzangu kwa kupoteza game ya Jana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…