Kocha wa Simba agoma kupangiwa kikosi na kiongozi wa juu

mkolaj

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2014
Posts
3,023
Reaction score
1,089
Hali inayosemekana kuwa timu zetu kongwe za kariakoo jijini dar es salaam kuwa na tabia ya viongozi wa timu hizo kuwapangia makocha wachezaji wa kucheza match, leo hii kupitia kituo cha redio cha PRIDE FM YA MTWARA kwenye kipindi cha michezo kimetoa taarifa kuwa kocha mkuu wa simba Goran Kopunovic amempiga mkwara kiongozi wa juu wa timu hiyo ndugu GOERFREY NYANGE KABURU kuacha tabia ya kumpigia simu ya kumwambia asiwapange baadhi ya wachezaji kwenye wanazocheza wekundu hao wa msimbazi. Baadhi ya wachezaji ambao KABURU amekuwa akiwataja ili wasipangwe ni Hassan Isiaka, Said Hamisi Ndemla na Mohammed Hussein Tshabalala. Kwa style hii ya viongozi wa timu zetu za bongo kuwapangia makocha wachezaji wa kucheza kwenye match wala tusitarajie mabadiliko yoyote kwenye mchezo wa mpira wa miguu. Hivi kweli kaburu ana sababu za msingi za kuwakataa hawa wachezaji wasipangwe kwenye match wanazocheza simba!!!!!
 
Hii habari nimeiona jana kwenye blog ya Bin Zubeiry, cha ajabu asubuhi hii sijaiona sijui kwa nini imeondolewa.
 
Hii habari nimeiona jana kwenye blog ya Bin Zubeiry, cha ajabu asubuhi hii sijaiona sijui kwa nini imeondolewa.
Ndugu bado hujajua tu!!!
Geofrey Nyange Kaburu na Zakalia Hans Pope ni kitu kimoja, bin zubeiry anamtegemea hans poppe ili mkono uingie kinywani je, unategemea nini hapo!!!
 
Ndugu bado hujajua tu!!!
Geofrey Nyange Kaburu na Zakalia Hans Pope ni kitu kimoja, bin zubeiry anamtegemea hans poppe ili mkono uingie kinywani je, unategemea nini hapo!!!
Ni kweli na hao jamaa ndio tatizo hasa pale Simba, na kama m/kiti ataendelea kuwalea kwa kuogopa kwamba wana hela atajikuta hata hela ya viingilio inapungua, nani anataka kwenda uwanjani kupoteza hela yake huku timu inafungwa.
 
wacheni kutuvuruga mwaujua moto wa Simba?
 
Ni kweli na hao jamaa ndio tatizo hasa pale Simba, na kama m/kiti ataendelea kuwalea kwa kuogopa kwamba wana hela atajikuta hata hela ya viingilio inapungua, nani anataka kwenda uwanjani kupoteza hela yake huku timu inafungwa.

Mkuu mbona tupo wengi tu ambao tuko tayari kulipa hata mara mbili ya viingilio vya kawaida ili tuone THIMBA KOKO inavyofungwa!?
 
Tatizo simba kila kiongozi ana mchezaji wake, ndio maana yanatokea haya. Ngoja timu ishuke daraja ndo watanyooka.
 
hizi hbr zimekaa kimajungu majungu tu. na wachangiaji weng hapa ni mayanga ushirikina club. Simba Tukitaka tunashinda tusipotaka tunaendelea kucheza kwa starehe tu.
 
Mipira ya kibongo bado sana that why watu wanakimbilia EPL, La Liga etc
Mie #TeamSimba lkn hii miendendo ya vilabu vyetu sio kabisa at least kidooooogo Lambalamba
 
Ukiona hivyo ujue hao wachezaji wamemgomea kumpa % f'lan ya mishahara yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…