Kocha wa Simba arejea Tanzania akitokea kwao Brazil

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2020
Posts
8,542
Reaction score
18,340
KOCHA wa Simba, Mbrazili, Roberto Oliveira ‘Robertinho ametua Dar es Salaam leo usiku na atakuwa mazoezini asubuhi kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida Big Stars Ijumaa.

Kocha huyo inaelezwa pia alihudhuria kozi fupi Ukocha kuongeza ujuzi nchini Brazili ingawa hajafafanua ilikuwa na levo gani.

Robertinho aliondoka nchini kwenda Brazil muda mfupi baada ya kukiongoza kikosi ushinda bao 1-0, dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma, amekosekana kwenye mchezo mmoja wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) timu yake ikipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union na kutinga hatua ya 16 bora.
 
Kocha makini sana, piga benchi yeyote timu isitegemee mtu mmoja siku akizingua mnalala na viatu. Tumpe muda aijenge timu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…