Kocha wa Simba na sub za kizamani

Kocha wa Simba na sub za kizamani

Justine Marack

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2014
Posts
612
Reaction score
1,698
Mimi sio Mchambuzi wala Kocha, natoa maoni yangu kwa uzoefu ninaoona kwa kile kinachofanywa na makocha wengine.

Katika mchezo wa jana Ahly na Simba, Sub ya Kenedy ilikuwa sub muafaka kwa wakati sahihi, lakini nimeona makocha wengi wakitaka kuzuia, nasi option ya kwanza ni kumiliki mpira.

Sasa kwa jana nilitarajia option ya kwanza ingekuwa kumuingiza Mzamiru ili kufanya pale kati Simba wamiliki dimba kwa kusaidiana na akina Ngoma na Kanoute, pale Mzamiru angafanya mchezo kurudi kwa Simba. Option ya pili ndio hiyo ya kuingizwa beki kama Kenedy.

Kitendo cha kuingia Kenedy inamaana kuwa Kocha alitaka kuwazuia Ahly katika mstari wa nyuma mbele ya lango. Hii ni kuwa unakaribisha mashambulizi dhidi ya wachezaji wenye quality kama wale Waarabu.

Yote kwa yote Mchezo ulikia mzuri. Hongera Robertinho.
 
Haikuwa sub nzuri na uko sahihi binafsi nisingefanya sub kabisa isipokuwa ningeongeza kelele kwa Chama na foward line waendelee kukabia juu
 
Kocha kimsingi alifaulu kimipango,Tatizo ni wachezaji walimwangusha hawakujituma kulinda mipango ya Kocha. Mfano namna ya kutumia chances wakipata mipira Hususani washambuliaji ilikua hovyo sana. Yaan mchezaji anajigongangonga tu miguuni mwa Al Ahaly hata pale anapokua na uwezekano wa kugawa pasi hatarii.

Simba Baada ya kuwafunga wangetuliza akili,ikiwezekana kupiga mipila kwao tu kuepuka kupoteza Moira kwa mpinzaniii.Game plan wali win ila fighting spirit ipo chiniii pia baadhi wachezaji uwezo upo chinii
 
Baada ya Al ahly kufungiwa walikuwa na kazi mbili kusawazisha na kuzuia wasifungwe. Kocha wetu alifanya sub iliyowasaidia na kuwapa kazi moja tu ya kusawazisha. Sub aliyofanya ingefanywa dakika za 80 ingekuwa nzuri zaidi kwa sababu tulikuwa tunawashambulia Sana.
 
Nimesema mara nyingi hapa jamvini Robetino muoga sana. Hata kwenye ligi akiwa na tofauti ya goli moja hata kama ni dakika ya 70 anakimbilia kujilinda kwa kuingiza kiungo au beki na kutoa mshambuliaji hata kama kakamata mchezo. Hii ni hatari sana. Makocha wenzake wote waliopita Simba walikuwa wanahakikisha kwanza wanampiga mtu goli za kutosha mapema halafu kuanzia dakika ya 70 inakuwa pira biriani. Kwa Robertino kuanzia dakika ya 70 mpaka mpira uishe utakuta mashabiki wa Simba wanaminya sehemu za siri, waliopo majumbani wanazima TV na redio zao.

Mechi ya AL AHLY Simba walitakiwa waingize winga/mshambuliaji mwenye kasi kwa sababu jamaa walikuwa wameshachoka na wamechanganyikiwa na lile goli la kushtukiza nina hakika "counter" moja tu Simba wangepata bao la pili. Kitendo cha kurudi kukabia nyuma kiliwapa jamaa utulivu na kuweza kusogelea lango la Simba na wakaweza kusawazisha kwa kuwa Simba ilikuwa na wachezaji wengi nyuma wanakabia kwa macho huku wakitegeana nani aokoe
 
Tatizo mnaangalia soka la ulaya Kisha mnakuja kulinganisha na hili pira la kikwetu kwetu, hao wachezaji mnaowataja na hayo majukumu mliyotaraji wayafanye ni vitu viwili tofauti
 
Kocha kimsingi alifaulu kimipango,Tatizo ni wachezaji walimwangusha hawakujituma kulinda mipango ya Kocha. Mfano namna ya kutumia chances wakipata mipira Hususani washambuliaji ilikua hovyo sana. Yaan mchezaji anajigongangonga tu miguuni mwa Al Ahaly hata pale anapokua na uwezekano wa kugawa pasi hatarii.

Simba Baada ya kuwafunga wangetuliza akili,ikiwezekana kupiga mipila kwao tu kuepuka kupoteza Moira kwa mpinzaniii.Game plan wali win ila fighting spirit ipo chiniii pia baadhi wachezaji uwezo upo chinii
Timu inaweza kucheza na No.6 wawili lakini kucheza na No.5 wawili ni uzushi. Anachosema mleta mada yuko sahihi. Ukifanya hivyo wote watakabia chini na mwisho watagongana ndani ya eneo au watategeana na ndicho kilichofanyika Jana kwenye tukio moja na kwenye goli la kisawazisha. Aliyetengeneza soka upande wa Idadi ya Wachezaji alitumia akili Sana. Kuna namba Wachezaji hawawezi kuwa wawili.
 
Mimi sio Mchambuzi wala Kocha, natoa maoni yangu kwa uzoefu ninaoona kwa kile kinachofanywa na makocha wengine.

Katika mchezo wa jana Ahly na Simba, Sub ya Kenedy ilikuwa sub muafaka kwa wakati sahihi, lakini nimeona makocha wengi wakitaka kuzuia, nasi option ya kwanza ni kumiliki mpira.

Sasa kwa jana nilitarajia option ya kwanza ingekuwa kumuingiza Mzamiru ili kufanya pale kati Simba wamiliki dimba kwa kusaidiana na akina Ngoma na Kanoute, pale Mzamiru angafanya mchezo kurudi kwa Simba. Option ya pili ndio hiyo ya kuingizwa beki kama Kenedy.

Kitendo cha kuingia Kenedy inamaana kuwa Kocha alitaka kuwazuia Ahly katika mstari wa nyuma mbele ya lango. Hii ni kuwa unakaribisha mashambulizi dhidi ya wachezaji wenye quality kama wale Waarabu.

Yote kwa yote Mchezo ulikia mzuri. Hongera Robertinho.
Uko sahihi kabisa ..nilikuwa .tu kwanza kusema hiki haja...
Baada ya kuongoza , ni sahihi kumtoa CHAMA, Pengine si mtu wa kubanana..
Kwa namna ambavyo Al Ahyl walivyokua wametawala kwa maahumbukizi ya mara kwa mara ...ilihitahika kujaza viungo ili kukata mashambulizi, hasa kiungo ambaye angeweza kurudi nyuma haraka kusaidia defence..
Palijitajika kuziba njia , ...na hapa nikimuona MZAMIRU
 
Kwakweli Jana wachezaji Simba wapewe maua Yao lakini benchi la ufundi walituuza
 
Hamna kocha mule... Yule ni msimamizi tubwa mazoezi.
Kuanza na boko tu, vyeo vyoote unamvua.
 
Back
Top Bottom