kombaME
JF-Expert Member
- Aug 24, 2015
- 2,115
- 2,818
Kocha wa simba, ndugu Patrick Winand J. Aussems, aliyezaliwa tarehe 6 February 1965 huko Moelingen, Ubelgiji. Huyu bwana hatajwi sana kwenye mafanikio ya simba, wanasimba wanawataja sana akina Kagere, Chama, Nyoni muda mwingine Manara n.k wakiwapa sifa kwamba hao ndo chachu kubwa ya ushindi wa wanamsimbazi hao, lakini huyu ndugu amekuwa sio wa maneno mengi, ni mtulivu aliyejikita zaidi Kwanye kujenga timu na kuleta matokeo chanya, kwangu ndo kocha bora katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kati.
Huyu bwana amewahi kucheza mpira, na enzi zake alikuwa anacheza nafasi ya ulinzi, na moja ya klabu kubwa ambayo amechezea ni Standard Liege ya nchini Ubelgiji, klabu zingine alizochezea ni pamoja na RCS Vise', K.A.A Gent, R.F.C Seraing zote za Ubelgiji na EA Troyes AC ya ufarasa.
Ameshawahi kufundisha vilabu vingi pamoja na timu ya Taifa, moja ya timu ya Taifa ambayo amewahi kuifundisha ni Benin na Nepal ambayo aliifundisha mwaka 2015-2016, Klabu alizozifundisha ni pamoja na Marbela United ya Hispania, AC Leopard ya Congo.. zingine ni CD Tiancheng na SZ Rubby, na klabu nynginezo nyingi hapa Afrika.
Huyu jamaa ameiwezesha kuifikisha Simba Sc robo Fainali, na kuifanya simba kuwa moja ya klabu kubwa barani Afrika, kutokana na mpira anaoufundisha ukavutia mashabiki wengi uwanjani na kuifanya klabu ya simba kuwa ndo klabu iliyojaza mashabiki wengi zaidi katika mashindano haya ya vilabu bingwa Afrika kwa msimu huu.
Kwa namna yoyote huwezi kuisifia simba ukamuacha huyu kocha mkubwa kabisa Afrika mashariki na kati na Afrika kwa ujumla.
Droo ya robo fainali tayari na Simba amepangiwa kigogo cha soka Afrika TP mazembe, je Aussems unadhan anatakiwa atumie approach ipi, aongeze nini au apunguze nini ili kuifanya simba SC iende nusu Fainali??
Sent using Jamii Forums mobile app