Kocha wa Simba Roberto asepe

covid 19

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
6,967
Reaction score
17,452
Mpira anaocheza simba ni wa hovyo na ni style ya huyu mwalimu mpya Roberto.

Wachezaji wapo ila hawapangwi ktk sehemu zao wachezaji wana struggle sana kucopy style ya kocha huyu na hawapo teyri.

Yanini kung'ang'ania mfumo usioendana na style ya wachezaji waliopo.

Kwa kikosi cha simba kama mgunda ndio angepanga team leo tulikuwa na uhakika na goli zaidi ya 3 pale..

Kwa hili linaloendelea nashauri huyu kocha aondoke tu atuachie team yetu isee.
 
Simba ya msimu huu ni makapi kabisa timu haina wachezi bora wengi wamechoka na hawajitumi kuitafutia timu matokeo
 
Wachezaji wazee wale,atafutiwe wachezaji,apewe muda
 
Yaa Yaan MO anasajili wachezaji.Anasajili kocha.Halafu anaonga waamuz.Du!!Tanzania tutalisikia tu kombe la dunia .
 
Mchezaji gani mzuri kaachwa Nje jana?
 
Kocha anaoenewa bure. Kwa nini mnakimbia ukweli kuwa Simba haina mshambuliaji makini namba tisa? Hivi yale magoli aliyokosa Saidoo mawili na Sakho moja ya wazi kabisa mlitaka Robertinho aingie afunge. Halafu wachezaji wanatembea tu na mpira uwanjani kama wameshinda goli 10 wakati wanaongoza goli moja ambalo linaweza rudi muda wowote. Kiufupi sana uozo ulianzia wakati wa usajili.

Pili Simba toka wamemuondoa yule kocha wa viungo Zarane (sijui nimepatia jina) timu nzima haina fitness. Ikifika dakika ya 60 wachezaji wote hoi wanabaki kukaba kwa macho. Mchezaji ambaye anaweza kucheza dakika 90 zote pale Simba ni Kibu Denis pekee pamoja na mapungufu yake mengine uwanjani.
 
Kazadi aliuwasha moto Mapinduzi,akaipiga goli nne Azam peke yake,akatupia tena na tena.

Alishakuwa AS Vita akatupia vya kutosha.

Kaenda Morocco katupia

Kaja ligi kuu sidhani hata kama ana goli moja. Tungekuwa hatujamuona Zanzibar na AS Vita tungelaumu sana Viongozi wa Singida BIG STARS
 
Kushinda sio issue ila ubora wa team hakuna kabisa huoni mipango kabisa.
Ubora wa timu kiuchezaji au ubora wa timu ki-wachezaji?

Na vipi ukilinganisha wachezaji na uchezaji wao? Bado huyo Robertinho ana kosa?
 
Ubora wa timu kiuchezaji au ubora wa timu ki-wachezaji?

Na vipi ukilinganisha wachezaji na uchezaji wao? Bado huyo Robertinho ana kosa?
Team hii hii ndio mgunda alivuka nayo group stage na mpira ulikuwa mzuri sana iweje leo mpira ubadilike ghafla baada ya kuja Roberto..

Jibu lipo wazi kocha Roberto ameleta mfumo mpya ambao ni mgumu kwa wachezaji wanatruggle sana uwanjani.
 
Team hii hii ndio mgunda alivuka nayo group stage na mpira ulikuwa mzuri sana iweje leo mpira ubadilike ghafla baada ya kuja Roberto..

Jibu lipo wazi kocha Roberto ameleta mfumo mpya ambao ni mgumu kwa wachezaji wanatruggle sana uwanjani.
Hivi kocha anatakiwa kuendana na wachezaji au ni wachezaji ndio wanatakiwa kuendana na kocha?

Mpaka uongozi unamteua kwa kazi, maana yake taarifa zake wanakuwa Nazo, na style ya ufundishaji wake inakuwa inajulikana.

Tatizo lenu Simba, hamuamini katka mabadiliko. Muda unaenda, ila wachezaji tegemezi ni wale wale, na mnataka waperform vilevile, kitu ambacho sio sawa.
 
Tanzania hatuamini katika sisi

Tunaamini kocha kutoka nje ndio bora kulinganisha na kocha wa ndani- hakukuwa na sababu ya kumsajili kocha mpya na wakati timu ipo nusu ya msimu au nusu na robo ya msimu kuisha ilihali kuna kocha japo sio rasmi lakini anaiongoza timu vizuri

Sio mbaya kumsajili kocha mpya ila wangemuachia kwanza Mgunda amalizie huu msimu wote na wangemsajili Robatinho aangalie picha jinsi mgunda anavyofanya nae asitie neno lolote na asome mchezo msimu ukiisha aanze kazi yake

Wamemkosea mgunda na hii itawagharimu

Kocha anasajiliwa kutoka nje!! analipwa pesa nyingi mno na afanyi vizuri means wat

Tim ilikuwa ya mgunda na ingeweza kufanya vizuri
 
Afu ukute anayesema hivyo hajawahi changia chochote Simba
 
Scars Kalpana denooJ OKW BOBAN SUNZU Ghazwat ....
 
Inafurahisha kuona kuwa pamoja na ushindi lakini hamna FURAHA.
 
R
Yule coach hana issue wachezaji ni wazuri ila mfumo wa Roberto unawatesa sana.
Robertinho mfumo wake ni kupress na kasi,kitu ambacho Kwa wazee wa Simba hawawezi,kumbuka vipers iliyocheza na yanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…