Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,703
- 1,724
Katika kukidhi maombi ya wananchi kutaka timu ya soka ya Taifa letu iwe na kocha mzawa, TFF imemteuwa C. B. Mkwasa kuwa kinara wa benchi la ufundi.
Kinachonitatiza ni kuwa kocha huyu bado ni kocha msaidizi wa klabu ya Yanga mpaka sasa. Hivi kwa mtu timamu utawezaje kutekeleza mipango ya klabu na taifa kwa wakati mmoja? Tusidanganyane.
Tunaona toka mataifa yanayofanya vizuri kisoka hayana 'usanii' huu. Juzi kaita wachezaji kwenye kambi ya mazoezi kwa timu ya taifa ambayo haina mechi yoyote ya kucheza, mie nikagundua ni njama yake ya kuidhoofisha timu ya Azam kwenye mechi ya Ngao ya hisani kwani itapambana na timu yake ya Yanga na yeye akiwa kwenye benchi la ufundi.
Aksante kwa viongozi wa timu ya Azam kwa kutowaruhusu wachezaji wake kuingia katika mtego huo.
Kwa mtindo huu nina uhakika timu yetu ya Taifa haitofika kokote.