Kocha wa soka timu ya Taifa, TFF karamu mbili zilimshinda fisi!

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Katika kukidhi maombi ya wananchi kutaka timu ya soka ya Taifa letu iwe na kocha mzawa, TFF imemteuwa C. B. Mkwasa kuwa kinara wa benchi la ufundi.

Kinachonitatiza ni kuwa kocha huyu bado ni kocha msaidizi wa klabu ya Yanga mpaka sasa. Hivi kwa mtu timamu utawezaje kutekeleza mipango ya klabu na taifa kwa wakati mmoja? Tusidanganyane.

Tunaona toka mataifa yanayofanya vizuri kisoka hayana 'usanii' huu. Juzi kaita wachezaji kwenye kambi ya mazoezi kwa timu ya taifa ambayo haina mechi yoyote ya kucheza, mie nikagundua ni njama yake ya kuidhoofisha timu ya Azam kwenye mechi ya Ngao ya hisani kwani itapambana na timu yake ya Yanga na yeye akiwa kwenye benchi la ufundi.

Aksante kwa viongozi wa timu ya Azam kwa kutowaruhusu wachezaji wake kuingia katika mtego huo.

Kwa mtindo huu nina uhakika timu yetu ya Taifa haitofika kokote.
 
Mi nashangaa sana yaani watz sasa wanavyojipa moyo juu ya timu yetu ya taifa kana kwamba kuna maboresho makubwa sana yamefanyika na kuifanya timu kuwa nzuri sasa kuna SLOGAN (silaha tumeweka chini)!!

mpira hauchezwi kwa slogan jamani, wachezaji ni wale wale kocha ni huyo mkwasa, ndio kujipa matumaini makubwa eti yakuitoa nigeria kwa mpira gani?? mpira ni sayansi na si siasa jamani!! tena kama radio E-FM!! imekuwa kama ni radio ya tff kwa ajili ya propaganda!!!

Tatizo la mpira wetu ni zaidi ya kocha.
 
E-fm wao hawana kosa wanajaribu kutia hamasa na kuitia mioyo ya watanzania kwenda uwanjan na kushangilia timu yao,cos mshabiki ni mchezaji namba kumi na mbili,tff na bench lake la ufundi ndio wapambana na timu,mashabiki tunaenda uwanjan kuwapa moyo vijana
 
Mkuu, angalia wanafiki walivo. Makocha wa kigeni kwenye vilabu vyetu hawapigiwi kelele ila kwenye timu ya Taifa tu. Nimegundua baada ya serikali kutia mguu wake wa kumlipa mshahara kocha wa timu ya Taifa ya soka basi wajanja wakaanza kuchonga 'uzawa'. Hiyo radio si ndo Maulidi Kitenge kahamia huko baada ya kutemwa Radio One? Mie ilifika pahala nikawa nakichukia kipindi cha "sporti leo" cha Radio One kwa ajili ya huyo mtangazaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…