Kocha wa Taifa Stars, Etienne Ndayiragije afungashiwa virago vyake

Kwani hawakuchukuliwa?
Walichukuliwa ila kuna walio achwa wenye uwezo tu wakachukuliwa wengine wenye uwezo mdogo kutoka mbwinde huko ili ionekane timu imeballance na jamaa aridhike ili kocha aendelee kulinda kibarua chake....

Sasa waliomjaza ili amfurahishe jamaa wamemtoa kafara ili wajisafishe....
 
Mpira nidhamu, bila nidhamu hakuna maendeleo.

Hao wavuta bangi mnao wategemea walete maajabu uwanjani, mtasubiri sana.
 
Nchi ya kipumbavu sana hii....aliyeamuru wasichukuliwe wachezaji wa Simba na Yanga anajulikana...watu wanajifanya kufukuza kocha...huu unafiki hadi lini nchi hii? kwanza kajitahidi kupata point nne huko CHAN.
Hao wa Simba na Yanga miaka zaid ya 50 wameshiriki mashindani, ni nini wamewahi kuleta kama mafanikio. Ushabiki mwingine unamfanya mtu aonekane wa ajabu sana
 
Nchi ya kipumbavu sana hii....aliyeamuru wasichukuliwe wachezaji wa Simba na Yanga anajulikana...watu wanajifanya kufukuza kocha...huu unafiki hadi lini nchi hii? kwanza kajitahidi kupata point nne huko CHAN.
Kwani hao wachezaji wa simba na Yanga walishafanya maajabu gani???

Tatizo hatuna mising ya football na michezo mingne full stop.
 
Hao wa Simba na Yanga miaka zaid ya 50 wameshiriki mashindani, ni nini wamewahi kuleta kama mafanikio. Ushabiki mwingine unamfanya mtu aonekane wa ajabu sana.
Acha kushikwa masikio na wachambuzi maandazi,jitahidi kuwa na mawazo yanayojitegemea.
Yaani uache wachezaji wazuri kisa wanacheza Simba Azam na Yanga?Uache bunduki utoke na rungu kisa vita iliyopita ulishindwa?sitaki kuamini kama uwezo wako wa kufikiri ndo umekomea hapo.
 
Atakuja mwingine tena naye tutafukuza...

Ishu ni kwamba hatujui mpira...full stop
 
Kwani hao wachezaji wa simba na Yanga walishafanya maajabu gani???

Tatizo hatuna mising ya football na michezo mingne full stop.
Ndo mawazo yako yameishia hapo? kwamba kama pombe haijakulewesha ni bora ujaribu kulewa maji? huoni hayo ni mawazo mgando na utakunywa bahari nzima bila kulewa.
 
Nimekuuliza, miaka yote 50 wametuletea mafanikio gani? naomba jibu. Katika uzuri wao unaouona, miaka hiyo yote nime mfano wa mafanikio waliotuletea kama nchi kwa kipindi chote hicho
 
Nimekuuliza, miaka yote 50 wametuletea mafanikio gani? naomba jibu
Swali lako halina uhalali wa kujibiwa unless unithibitishie kuwa hao wachezaji A walikua wanakwenda mashindanoni kuleta mafanikio ambayo wachezaji B wameshindwa kuyaleta,lakini hao hao wachezaji B ndo waliofuzu kwenda huko CHAN.
 
Tatizo Tff wanapenda kitonga hivi walishindwa kutangaza nafasi mpaka wanachukua kochakwa mfumo wa kuokoteza
 
Swali lako halina uhalali wa kujibiwa unless unithibitishie kuwa hao wachezaji A walikua wanakwenda mashindanoni kuleta mafanikio ambayo wachezaji B wameshindwa kuyaleta,lakini hao hao wachezaji B ndo waliofuzu kwenda huko CHAN.
Kwaiyo kama hawajaleta, kwani wengine wakienda kuna tatizo gani? Au wao siyo watanzania ilawale tu wa simba na yanga? Dunia ya soka sasa hivi ni mafanikio,kama hakuna kwanini tuzidi kuwatumia wao? Au wao ndo wana uhalali wa utanzania zaidi kuliko vilabu vingine? Simaanishi kukubaliana kwamba mtu asichukuliwe sababu tu anachezea timu flani, lakini pia siyo kwa kuwa anachezea timu flani basi yeye ndo anastahili.
 
Nimekuuliza, miaka yote 50 wametuletea mafanikio gani? naomba jibu. Katika uzuri wao unaouona, miaka hiyo yote nime mfano wa mafanikio waliotuletea kama nchi kwa kipindi chote hicho
Walituletea challenge [emoji85]
 
Basi itakua hukunielwa hapo awali...nilichosema ni kuwa kuna wachezaji wameachwa kwa sababu wanacheza club hizo kubwa lakini si kwa sababu ya uwezo.....suala siyo wachezaji wa timu kubwa kuachwa suala ni w achezaji wenye uwezo kuachwa kisa wanacheza timu fulani ili kuweka ballance kitu ambacho si sawa.
 
Mkuu, unakosea mno. Wachezaji walijituma sana kwa heshima ya nchi, kilichokuwa kinakosekana ni ujuzi wa benchi la ufundi.
Hivi akina Nchimbi wanabakia na goalkeeper wanapaisha, hapo ni uzoefu gani unahitajika kutoka bench la ufundi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…