Kocha wa Taifa Stars jitafakari

Kocha wa Taifa Stars jitafakari

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2016
Posts
2,668
Reaction score
3,751
Leo timu ya taifa ( taifa stars) imenyolewa kwa chupa mbele ya watanzania pamoja na hamasa iliyokua uwanjani na mitandaoni

Binafsi siamini katika hamasa kuliko kujishuhulisha.

Imewezekanaje mpira uliopigwa leo na Taifa stars ichabangwe goli mbili kwa buyu? Tena mbele ya waziri mkuu Majaliwa na mzee Jakaya Kikwete . Hii ni aibu kubwa sana na ndio maana watu wanaona bora washabikie Simba na Yanga kuliko kutonesha mioyo yao kila siku.

Kocha gani asiye badilika? Kama wazawa hawawezi sasa ndio iwe kweli Taifa Stars ni KICHWA CHA MWENDAWAZIMU kila anaetaka kujifunza kunyoa anapewa nafasi?

Mtazamo wangu nikwamba

1: Kuna kasumba ya usimba na uyanga ndani ya timu ya taifa. Kwanini wachezaji kutoka klabu nyingine kama coastal, Singida n.k hawajaitwa?

2: Kuna ugonjwa wa kuamini majina yaleyale kila siku kuliko kuongeza nguvu kwa wachezaji au majina mageni kwenye timu yetu ya taifa. Mbona Awesu hamjamuita? Au anacheza chini ya kiwango?

3: Kukosekana kikosi kipana kwa timu ya taifa imekua tatizo na niaibu ambayo inamuelemea kocha.
4: Nikwanini serikali isiajiri kocha mwenye weledi,asiyefanya kazi kwa hisia badala yake aendane na uhalisia? Unakuaje na kocha wa timu ya taifa ambaye kikosi chake kinatabirika? Yaani hakuna hata wachezaji wa kufanyiwa mabadiliko? AIBU YAKO KUBWA SANA KOCHA NA BENCHI LAKO LA UFUNDI. AIBU KWENU TFF

Soma Pia: Full Time: Tanzania 0- 2 DR Congo | Qualification AFCON 2025 | Benjamin Mkapa Stadium | 15 Oktoba, 2024
 
Shida mnamzonga sana mara hajamchezesha furani... Baadae anaanza kufata makelele yenu
Kwanza nawashangaa kumlaumu kocha binafsi sijawahi kushuhudia nyakati nzuri Kwa Taifa stars zaidi sana enzi ya Marcio Maxime the rest ni majanga tuu ndio maana sishabikiagi Hilo litimu bovu la wakati wote
Naipenda Yanga shabiki wa damu
 
Kocha anaangalia majina ya Kiislamu tuu ndo unaitwa hata Kama hujui kucheza! Kiufupi hatufai hatufai.... Unamwachaje Kelvin John, unamwachaje Msuva, unamwachaje Awesu, unamwachaje Balua
Hii sasa naamin huko kunakuaga na kama kutoa takrima ili upewe namba mana sielewagi kabisa unaaacha wachezaj wazur unaita mafamba akina samata ..na zaid wanaongeza na siasa....anyway wamuajiri alio cisse si kaachwa senegal, labda kwa project ya muda mfupi ili 2027 tusikose
 
Hapo kwenye takrima pana hoja ya msingi
Kwa takrima hatutotoboa
 
Kocha anaangalia majina ya Kiislamu tuu ndo unaitwa hata Kama hujui kucheza! Kiufupi hatufai hatufai.... Unamwachaje Kelvin John, unamwachaje Msuva, unamwachaje Awesu, unamwachaje Balua
Halafu mtu anakaa hana wachezaji wa kubadilisha
Natamani achapwe viboko hadharani
 
Kocha na tff wajiuzulu tofauti na hapo maneno ya Mzee Mwinyi yataendelea kudhibitishwa
 
Kocha anaangalia majina ya Kiislamu tuu ndo unaitwa hata Kama hujui kucheza! Kiufupi hatufai hatufai.... Unamwachaje Kelvin John, unamwachaje Msuva, unamwachaje Awesu, unamwachaje Balua
Awesu na kelvin walitakiwa wawepo
 
Mmeanza kumtupia lawama kocha.kwahiyo wewe uliamini timu ya hamasa za kisiasa badala ya uwezo wa kimpira inaweza ikaifunga Drc.Kocha hana shida na wachezaji hawana shida.Hicho ndio kikosi chetu cha mwisho na uwezo wetu ulipoishia.Hatuna maajabu yoyote zaidi ya porojo za mdomoni.
 
Leo timu ya taifa ( taifa stars) imenyolewa kwa chupa mbele ya watanzania pamoja na hamasa iliyokua uwanjani na mitandaoni

Binafsi siamini katika hamasa kuliko kujishuhulisha.

Imewezekanaje mpira uliopigwa leo na Taifa stars ichabangwe goli mbili kwa buyu? Tena mbele ya waziri mkuu Majaliwa na mzee Jakaya Kikwete . Hii ni aibu kubwa sana na ndio maana watu wanaona bora washabikie Simba na Yanga kuliko kutonesha mioyo yao kila siku.

Kocha gani asiye badilika? Kama wazawa hawawezi sasa ndio iwe kweli Taifa Stars ni KICHWA CHA MWENDAWAZIMU kila anaetaka kujifunza kunyoa anapewa nafasi?

Mtazamo wangu nikwamba

1: Kuna kasumba ya usimba na uyanga ndani ya timu ya taifa. Kwanini wachezaji kutoka klabu nyingine kama coastal, Singida n.k hawajaitwa?

2: Kuna ugonjwa wa kuamini majina yaleyale kila siku kuliko kuongeza nguvu kwa wachezaji au majina mageni kwenye timu yetu ya taifa. Mbona Awesu hamjamuita? Au anacheza chini ya kiwango?

3: Kukosekana kikosi kipana kwa timu ya taifa imekua tatizo na niaibu ambayo inamuelemea kocha.
4: Nikwanini serikali isiajiri kocha mwenye weledi,asiyefanya kazi kwa hisia badala yake aendane na uhalisia? Unakuaje na kocha wa timu ya taifa ambaye kikosi chake kinatabirika? Yaani hakuna hata wachezaji wa kufanyiwa mabadiliko? AIBU YAKO KUBWA SANA KOCHA NA BENCHI LAKO LA UFUNDI. AIBU KWENU TFF

Soma Pia: Full Time: Tanzania 0- 2 DR Congo | Qualification AFCON 2025 | Benjamin Mkapa Stadium | 15 Oktoba, 2024
Hamasa Stars ..
 
Pale nilipomsikia Msigwa redioni anapromote hii gemu nikazima redio na kujisemea, ***** tumekwishaaaaa....gemu zote serikali ilizoingiza promo zake 90% tuliangukia pua.
 
Back
Top Bottom