Anfaal
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 1,154
- 116
Kuna hili suala la kocha wa Timu ya Taifa kufundisha Kilimanjaro Stars wakati Zanzibar pia kuna timu nyingine.
Nadhani kuna haja ya kocha wa Taifa aendelee kubaki kuwa wa Taifa na michuano kama ya challenge ambayo haitambuliki na FIFA wawe wanapewa makocha wazalendo. Ni lini Taifa litajiaminisha kwa makocha wazalendo. Kama tunashindwa kuwapa hata nafasi katika michuano hii, lini tunawaamini. Pia michuano kama hii ingetumiwa maalum hasa kwa kocha kutafakari vipaji vilivyopo kutoka pande zoote mbili za nchi. Naomba nieleweke wazi kuwa posts hii haina malengo ya kisiasa.