Kocha huyo wa Cranes anaamini kikosi chake kinapaswa kuwalinda vizuri wachezaji wote wa Misri katika mchezo wao wa leo usiku.
Ugandan Cranes ilishinda mchezo wake wa kwanza nyumbani kwa bao 1-0 dhidi ya vijana wa Hector Cuper katika kusaka kwa Kombe la Dunia 2018.
“Tunakiheshimu kikosi chote cha timu ya taifa ya Misri. Hatukuja kucheza dhidi ya Mohamed Salah au Mohamed Elneny pekee,lakini tumejiandaa na kucheza na wachezaji 11 wa Misri,” alisema Basena.
====
Uganda watachomoka kwa waarabu kweli? Ninavowajua waarabu wana visa sana..Sitasahau siku Simba walichezaga na timu moja ya huko uarabuni na mchezo ulipigwa usiku. Ghafla mashabiki wakaanza kuwasha moto kandokando ya uwanja, sikuwaelewa kabisa. Waarabu wana visaaa