Kocha wa Uganda Basena awachimba mkwara Misri, adai hamuogopi Salah

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Cairo, Misri. Baada ya kutua Misri, kocha wa timu ya taifa ya Uganda, Moses Basena amesema hawataweka akili zao zote kwa Mohamed Salah au Mohamed Elneny.

Kocha huyo wa Cranes anaamini kikosi chake kinapaswa kuwalinda vizuri wachezaji wote wa Misri katika mchezo wao wa leo usiku.

Ugandan Cranes ilishinda mchezo wake wa kwanza nyumbani kwa bao 1-0 dhidi ya vijana wa Hector Cuper katika kusaka kwa Kombe la Dunia 2018.

“Tunakiheshimu kikosi chote cha timu ya taifa ya Misri. Hatukuja kucheza dhidi ya Mohamed Salah au Mohamed Elneny pekee,lakini tumejiandaa na kucheza na wachezaji 11 wa Misri,” alisema Basena.

====

Uganda watachomoka kwa waarabu kweli? Ninavowajua waarabu wana visa sana..Sitasahau siku Simba walichezaga na timu moja ya huko uarabuni na mchezo ulipigwa usiku. Ghafla mashabiki wakaanza kuwasha moto kandokando ya uwanja, sikuwaelewa kabisa. Waarabu wana visaaa
 
hii game ipo lini? nijuze mwenye kujua PLZ

Sent using Jamii Forums mobile app
Game ilikuwa jana usiku saa tatu Uganda alipigwa moja,,,,,kabla Okwi hajatolewa Uganda ilikuwa roho mkononi,jamaa hakuonekana kabisa,Uganda walikuwa wanashambuliwa kila muda kama siyo uimara wa Onyango wangepigwa tano.Walipomtoa Okwi ndo kidogo wakajimudu,hadi mwisho Misri moja Uganda sufuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashukuru mkuu.sijaona hayo matokeo kwenye mitandao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashukuru mkuu.sijaona hayo matokeo kwenye mitandao

Sent using Jamii Forums mobile app
Inaonekana watu wengi hawakufuatilia,,,,,Congo Brazavile yy alipigwa mkono na Ghana.Ila kiukweli Uganda wanajua mpira hizo point 7 walizonazo ni halali yao,wanapiga soka hatari,Okwi hana kitu wale madogo ni noma hata Juuko yuko vizuri mno sema akiwa Simba anafanya masihara labda haridhiki na malipo ila jamaa ni mzima vibaya au labda simba wanamchezesha nafas siyo yake.Waganda ni noma na Onyango ni balaa sijui anacheza wapi,anatakiwa kucheza first class clubs za Ulaya.Mpira ulikuwa mzuri asee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…