Kocha wa Yanga atoa silimia zake kwa timu ya Simba kushiliki lobo fainali

ChikoTz

Member
Joined
Feb 26, 2019
Posts
37
Reaction score
33
Mkongomana wa Yanga ambae ndiye Kocha Mkuu Mwinyi Zahera amefunguka na kuipa asilimia 60 klabu ya Simba kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Aidha ametoa asilimia 40 kwa klabu ya AS Vita kufuzu robo fainali katika kundi D ambalo lina timu zingine ambazo ni Al Ahly na JS Saoura.

Mkongomani huyo amedai Vita hata akishinda mchezo wake dhidi ya Al Ahly na Simba ikapoteza mbele ya Saoura bado itakuwepo.

Ameenda mbali zaidi na kusema kuwa Simba wana nafasi kubwa ya kushinda mchezo wa mwisho na kuweza kufuzu robo fainali dhidi ya Vita itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Tayari kikosi cha Simba kipo angani hivi sasa kikielekea Algeria kwa ajili ya mechi na Saoura ukiwa ni mchezo wa pili baada ya ule wa kwanza Simba kushinda mabao 3-1

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa anazungumzia wapi hayo maneno. Maana yamekuwa too much,au mnamvizia mzee wa watu akiwa anapiga gahawa?
 
Reactions: mmh
Usahihi Simba vs Js Saoura 12/01/2019 Matokeo yalikuwa 3-0(Okwi 45"Kagere 52"68") na sio 3-1
 
Yaani kama umesoma probability na mechi katika nchi za kiafrica basi Simba kishapita. Halafu sijui kwa nini Africa team ni ngumu sana kupoteza mechi za nyumbani. Siyo kama Ulaya jana tumeshuhudia Real akipigwa kwao 4.
 
Nionavyo huwa wanamlisha maneno Mzee wa watu bana.
 
Yaani kama umesoma probability na mechi katika nchi za kiafrica basi Simba kishapita. Halafu sijui kwa nini Africa team ni ngumu sana kupoteza mechi za nyumbani. Siyo kama Ulaya jana tumeshuhudia Real akipigwa kwao 4.
1)timu kujikakamua ili isiaibike mbele ya mashabiki.
2)UCHAWI. Mganga anaweza sema anataka kuweka kitu uwanjani kama,uwanja wa ugenini huwezi pata upenyo.
Mafanikio ya kimpira yanategemeana na parameters nyingi (Wachezaji Bora,kocha Bora,uwanja,utulivu wa akili(kulipwa on time),kuhonga marefa(case study Juventus 2007),udhaifu wa mpinzani.
Hata Ulaya Barca 2008,2009,2010 hajawahi pata matokeo ugenini. Chini ya Guardiola. UEFA.

Ndio maana goal la ugenini Lina heshima yake ,Away goals rule. Ni dunia nzima kushinda ugenini Ni ngumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…