Kocha wa Yanga, George Lwandamina: Mtibwa ni 'pasua kichwa' na wanajua kupambana

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
KOCHA wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, George Lwandamina, amesema kuwa mechi dhidi ya Mtibwa Sugar itakayofanyika kesho kwenye Uwanja wa Uhuru "si ndogo" kama ambavyo baadhi ya wadau wanavyoiangalia.

Akizungumza na gazeti hili jana, Lwandamina, alisema kuwa matokeo mazuri waliyonayo Mtibwa Sugar yanawasaidia kuondoa wasiwasi katika mechi itakayowakutanisha na hivyo anaamini itakuwa na changamoto zaidi kwa upande wake.


Lwandamina alisema kuwa anaamini uzoefu wa mechi za kimataifa na faida ya kucheza nyumbani ndiyo vitu anavyovitegemea kumsaidia kupata ushindi katika mchezo huo.

"Mechi dhidi ya Mtibwa Sugar ni ngumu na ya ushindani, ni moja kati ya klabu zenye wachezaji wanaojua kupambana," Lwandamina alisema kwa kifupi.

Kocha huyo wa zamani wa Zesco ya Zambia aliongeza kuwa anaamini wachezaji wake watapambana, ili wapate pointi zote tatu katika mechi hiyo na kukaa katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.

Mzambia huyo alifurahi kuona mshambuliaji wake wa kimataifa, Amissi Tambwe, anaendelea vyema na uamuzi wa kumpanga utajulikana kesho baada ya kumaliza mazoezi.

CHANZO: Nipashe
 
Hiyo mechi chini ya Lwandamina ni kubwa sana ila ingekuwa chini ya Pluijm hiyo ni mechi ndogo sana
 
 
Huyu kocha lwandamila utashangaa anamweka makapu,makapu mechi hii ngumu hawezi kuperform vizur hii game ,tunaitaji kushinda ili tuongeze point,yanga oyeeee!!!!
 
Uyu lwandamina aongee porojo zake ahakikishe yanga inashinda huu upuuzi wake sisi hatuutaki......kila la kheri yanga
 
Yanga kocha ninyule yule plujm huyu na tumbo lake hakuna kitu. Yanga sio yanga ilee.timu imepooza hakuna mashambulizi wala magoli mengi. Nakuhakikishia yanga ya mwala huu ni nzuri kuliko aloiacha babu shida hakuna kocha.
Mpeleke ngoma kushoto kama babu, ajibu kulia na chirwa katikati uone kama mtibwa hawafi mapema leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…