Kocha Zoran ampa onyo Kali John Bocco

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Kocha Zoran ameendelea kugawa dozi kwa wachezaji, huku akimkomalia Bocco, akimtaka kuchagua moja kati ya kucheza mpira na kubakishwa kambini au awafuate kina Meddie Kagere, Chris Mugalu na Taddeo Lwanga waliofyekwa Misri.

Inadaiwa Bocco amekuwa akitegea sehemu ya mazoezi ya timu na inadaiwa imemfanya kocha huyo kukaa naye na kumtaka achague kucheza au kama anasumbuliwa na majeraha basi atafutiwe matibabu haraka kabla ya kufanya uamuzi wa kubaki naye Msimbazi au kufyekwa kama alivyofanywa kwa kina Mugalu waliorejeshwa nchini.

Katika hatua nyingine kocha huyo amesisitiza anataka atafutiwe washambuliaji wawili akiwamo namba tisa wa ukweli kutokana dili na Cesar Manzoki kuonekana kukwama na kusubiriwa kuongezwa katika dirisha dogo, jambo litakaloifanya timu isiwe na straika wa kutegemewa.

Awali, ilitarajiwa dili la Manzoki likamilishwe kwa Simba kutuma kigogo kwenda kuzungumza na uongozi wa Vipers ya Uganda inayommiliki mchezaji huyo, lakini mambo yamekwama kwa sababu klabu hiyo ya Uganda inataka ilipwe Dola 200,000 miezi miwili iliyobaki ya mkataba wake.
 
Unataka kunambia huko mazoezin kibu d amekaza au Yuko Kambi ya taifa?
 
Mshambuliaji hatari Kibu Denis akiripoti kambini mapema, atasawazisha hayo makosa yote ya washambuliaji wenzake.
 
Kocha Zoran ameendelea kugawa dozi kwa wachezaji, huku akimkomalia Bocco, akimtaka kuchagua moja kati ya kucheza mpira na kubakishwa kambini au awafuate kina Meddie Kagere, Chris Mugalu na Taddeo Lwanga waliofyekwa Misr...
Boko kwa Umri alionao plus kuwa Kwake proin injury alipaswa awe ameshaagwa kwa Heshima na Simba SC nashangaa bado Uongozi upo nae tu. Manzoki anaweza Kutua Simba SC muda wowote Ndugu.
 
Waliotemwa rasm mpk Sasa HV Ni kina nani
 
Boco, Nyoni, Gadiel na Muzamiru Simba siyo size yao. Waondoke tu, akina Jamal Mnyate tulikuwa tunawaambia hiv hivi wakawa wanaona kama uonevu, huko walikoenda wamechemka vibayaaaaa
 
Acha Ramli chonganishi..chanzo cha taarifa yako?
 
Mkude kamwondoa yule Mbrazil na sasa Lwanga,huyu jamaa hafai kugombea nae namba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…