Kodi inakatwa Kwa watu wazalishaji, umri sio kigezo

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
KODI IKATWE KWA WATU WAZALISHAJI; UMRI SIO KIGEZO.

Anaandika Robert Heriel.

Serikali inayowajibu wa kutengeneza mazingira Kwa watu wake kujizalishia mali, serikali makini ni Ile inayofanya lolote, halali au haramu ili Raia wake wapate maisha Bora.
Niliwahi sema hapa, Bila kuvamia nchi zingine hakuna tutakachofanya Kwa ajili ya nchi yetu na wananchi wetu.
Tusipovamia mataifa mengine ili tuyafanyie unyonyaji na uharamia Nina uhakika Asilimia Mia moja kuwa tutavamiana wenyewe kwa wenyewe na kunyonya Raia na kuwafanyia uharamia ili kujenga nchi. Hata hivyo hakuna nchi iliyojengwa Duniani ikawa taifa la maana bila kuvamia mataifa mengine.

Niliandika hapa 👉👉 Tusipovamia mataifa mengine, tutaendelea kusumbuana. Serikali nisikieni Mimi

Kisha nikaandika andiko jingine hapa👉👉Bila uvamizi tutaendelea kukopa mpaka tuuze hii Nchi

Najua wapo watu wasioelewa namaanisha Jambo gani, wengine wananielewa lakini wanaona ni Jambo gumu pengine lisilowezekana,
Lakini hakuna Jambo gumu Kama kunyonyana Damu wenyewe Kwa wenyewe, hakuna Jambo gumu Kama Baba Kula nyama za watoto wake. Ni rahisi Sana kuvamia mataifa mengine na kuwatoa maoni, moyo, Firigisi huku wengine tukipasua kichwa ili tule Ubongo.

Mimi kwangu Hilo sio tatizo, najua Ndio Siasa na mambo ya Utawala, mambo ya mbugani ndio yako hivyo, tuchague Kula au kuliwa.

Kama ushauri wangu utapuuziwa, ni hakika tumeamua kulana wenyewe Kwa wenyewe Kama Samaki huko baharini, utitiri wa Kodi mpaka zisizo na maana yoyote zitaendelea kuibuliwa mpaka watu wakuone,
Too zaidi zitabuniwa ili kunyonya na kunyongana hasa Wale wasio na uwezo.

Zingatia, hata Kodi tutoe watu wote nchi nzima, kanuni ya Kulana nyama inasema; Mliwa nyama kamwe hapaswi Kula nyama yake.
Yaani watu hata wakamuliwe Kodi mpaka wazimie bado hawatafaidi matunda ya Kodi zao.

Kodi wanatakiwa watoe watu wazalishaji, kusema kigezo kiwe umri ni kichekesho 😀😀 cha Wala nyama ambao wanasema Kuku akifikisha umri wa kutaga sharti atage bila kujali wamempa chakula au hawanampa, wamempandisha jogoo au lash! Kinachotakiaa ni mayai.

Ni Sawa na Mungu adai Zaka na Sadaka Kwa mtu ambaye hajambariki chochote kwenye uzalishaji huo ni Uhuni.

Vijana wa sasa wanapitia kipindi kigumu alafu Badala ya serikali kujipanga namna ya kuwasaidia Yoo inapanga namna ya kuwala nyama,

Tusipovamia mataifa mengine;
Tutakulana nyama
Tutanyongana!
Tutageuzana Mishikaki
Tutapigana RISASI na Mikuki
Tutatekana na kufungana
Tutaitana wachawi na walozi,
Tutanyonyana Damu.

Wawekezaji ni muhimu lakini sio muhimu kama Sisi tukiwa wawekezaji zaidi ya wageni.
Serikali inashindwaje kutengeneza matajiri wazawa kuwa wawekezaji wakubwa mpaka tutegemee mataifa mengine kuja kuwekeza hapa.

Taikon anauhakika kuwa wapo watu wenzetu waliotunyonya Damu ambao wanamapesa mengi sana, Kwa nini serikali isiwajengee mazingira ya kuwekeza hapa ndani Kama wameshindwa kuwafunga Jela.

Kuvamiwa na wageni na kugeuzwa vibaraka, machawa na wakimbiza upepo wao ni Jambo linalofedhehesha,
Usalama wa taifa sharti ujue na uwe na moyo wa kizalendo sio tuu kulinda Amani ya nchi lakini pia kulinda maslahi ya nchi Kwa kuhakikisha kuwa Wageni hawatuvamii na kututawala.

Usalama WA taifa mtanijibu Mimi ndugu yenu; Nchi yetu Yale makampuni Makubwa, viwanda na matajiri wakubwa je ni watu wa nchi yetu au ndio tumevamiwa?

Sifurahishwi na kinachoendelea Kwa kweli, hakuna Jambo linaloniumaga na kuliona Kama laana, Kama kutawaliwa na mtu Mgeni, hata mkisema Mimi ni Mbaguzi wala hamtakuwa mmekosea, Mimi siogopi kubaguliwa nikiwa ugenini iweje nisiwe mbaguzi nikiwa nyumbani.

Hizo kodi bunifu na tozo umizi ni Kwa hawa vijana wanaolipwa 150,000 Kwa mwezi na kufanya kazi masaa yasiyopungua kumi na mbili, embu acheni utani.

Hizi Kodi ndio zipo Kwa ajili ya hawa house Girl na houseboy wanaolipwa elfu 50 come on!
Au ndio hawa Bodaboda au hawa Vijana wanaoranda Randa mitaani kubeti bila kazi ya maana?
Au ndio hawa wanawake kutwa kucha ninaowaona wakiombewa Kwa Manabii wa upako?

Kama mkinisikiliza basi tunaweza Anza na masuala Yafuatayo;
1. Boresheni Mazingira ya Kilimo yawe nafuu.
√ Toa mikopo,
√ Ondoa Kodi ya pembejeo, viwatilifu, na zana zote za kilimo.
√ Sambaza maafisa ugavi kila pembe ya nchi watoe elimu Kwa Wakulima.
√ Tengeneza mazingira ya njaa Kwa nchi tunazozimudu, iwe Kwa vita, au Kwa kutoa mazao yenye BEI nafuu ili mazao yetu yanunuliwe Kwa wingi kutokana na Wakulima kuzalisha Sana.

2. Ondoa upuuzi na watu wapuuzi kwenye Media.
Serikali izuie watu wenye akili ndogo kuonyeshwa kwenye media, na upuuzi wao.
Vijana tangu wakiwa wadogo waone mambo ya maana kwenye Vyombo vya habari, sio masuala ya kitoto toto na mambo Rahisi.
Hii itawafanya wasiwe na akili za kipuuzi puuzi.
Nikisema kuvamia tunavamia kiukweli kweli, na tunahitaji Vijana wenye akili za kutosha na wanaojua nini wanafanya.

Sio Vijana ambao hata ukiwapa kazi wanawaza mambo ya kipuuzi yanayofanywa na wapuuzi kwenye media.

Nilitembelea baadhi ya vyuo vya Kati na vyuo vikuu, nikashangazwa na Wanafunzi tena wengine WA masomo ya Udaktari wakiwa na mawazo na mtazamo Kama vile Waigizaji wa mambo ya upuuzi upuuzi tuu! Hii ni kutokana na kile wakionacho kwenye Vyombo vya habari.

Najaribu kusema upuuzi ndani ya nchi Kama unaofanywa na Wasanii sijui Kick sijui upupu gani ufanyike mara moja Kwa wiki iwe sehemu Kama ya vichekesho na jamii hasa Vijana wavichukulie Kama vituko na vichekesho, sio kila siku upuuzi tuu na vituko mwishowe Vijana wadogo watafikiri hayo ndio Maisha, nao tutakuwa na taifa la vituko, vichekesho na upuuzi tuu.

3. Vijana wafundishwe kuthamini wenyeji kuliko wageni.
Ni aibu na kujidhalilisha kumthamini Mgeni kuliko mwenyeji, ni Dalili ya kujiona Duni.
Sio ajabu Rais wetu hata akienda nchi za wenzetu usishangae hapewi mapokezi yanayomstahili, kumaanisha wanatudharau.
Lakini huku kwetu akija Rais yeyote hata Kwa mambo yake binafsi tunamshobokea.
Hili ni tatizo hata kwenye mazingira ya kazi, iwe ni polisi, marafiki, waalimu, madaktari n.k.
Mzungu au muarabu au mhindi akifika anapewa Huduma nzuri kuliko muafrika mwenzetu. Hiyo ni Akili za kitumwa.

Jambo Hilo linaanzia kwenye familia, wazazi tunaowajibu WA kuwafundisha watoto Jambo hili. Mwenyeji ni Bora kuliko Mgeni.

4. Nishati ya umeme isambazwe kila Nyumba
Usiseme pesa tutatoa wapi, huo ni ujanja ujanja. Kama pesa za kuiba zinapatikana ni upuuzi kuuliza pesa za kusambaza umeme zitapatikanaje na wapi.

5. Kusambaza Maji kila kijiji na kila nyumba.

Nimechoka! Acha nipumzike Sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Point watengeneze skim za umwangiliaji kila Wilaya na vijana wapate kazi, pia watafute masoko nje ya nchi ya kutosha kabisa
 
Bado taarifa hii ya Hali ya uchumi wa nchi ina mambo mazuri mengi tu. Hata hivyo, Kuna vichache vinafikirisha hivi:

"Kijana yupo Chuoni, anasoma anatakiwa kulipa kodi wakati anakopa fedha za kumsomesha Tena kwa riba!

Au mzazi anamsomesha mtoto CHUO, anatakiwa amlipie kodi. Kiasi fulani serikali kama inataka kutoza wazazi kodi kwa kupata watoto!( Sina hakika kama ina nia hii)"
 
Hii nchi tunaleana sana..watu walipe kodi kila mwenye umri wa miaka 18 alipe kodi kwa maendeleo ya nchi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Bado taarifa hii ya Hali ya uchumi wa nchi ina mambo mazuri mengi tu. Hata hivyo, Kuna vichache vinafikirisha hivi:

"Kijana yupo Chuoni, anasoma anatakiwa kulipa kodi wakati anakopa fedha za kumsomesha Tena kwa riba!

Au mzazi anamsomesha mtoto CHUO, anatakiwa amlipie kodi. Kiasi fulani serikali kama inataka kutoza wazazi kodi kwa kupata watoto!( Sina hakika kama ina nia hii)"
Neno 'kipato' hamlizingatii kabisa kwenye kauli ya mwigulu!
 
KODI IKATWE KWA WATU WAZALISHAJI; UMRI SIO KIGEZO.

Anaandika Robert Heriel.

Serikali inayowajibu wa kutengeneza mazingira Kwa watu wake kujizalishia mali, serikali makini ni Ile inayofanya lolote, halali au haramu ili Raia wake wapate maisha Bora.
Niliwahi sema hapa, Bila kuvamia nchi zingine hakuna tutakachofanya Kwa ajili ya nchi yetu na wananchi wetu.
Tusipovamia mataifa mengine ili tuyafanyie unyonyaji na uharamia Nina uhakika Asilimia Mia moja kuwa tutavamiana wenyewe kwa wenyewe na kunyonya Raia na kuwafanyia uharamia ili kujenga nchi. Hata hivyo hakuna nchi iliyojengwa Duniani ikawa taifa la maana bila kuvamia mataifa mengine.

Niliandika hapa 👉👉 Tusipovamia mataifa mengine, tutaendelea kusumbuana. Serikali nisikieni Mimi

Kisha nikaandika andiko jingine hapa👉👉Bila uvamizi tutaendelea kukopa mpaka tuuze hii Nchi

Najua wapo watu wasioelewa namaanisha Jambo gani, wengine wananielewa lakini wanaona ni Jambo gumu pengine lisilowezekana,
Lakini hakuna Jambo gumu Kama kunyonyana Damu wenyewe Kwa wenyewe, hakuna Jambo gumu Kama Baba Kula nyama za watoto wake. Ni rahisi Sana kuvamia mataifa mengine na kuwatoa maoni, moyo, Firigisi huku wengine tukipasua kichwa ili tule Ubongo.

Mimi kwangu Hilo sio tatizo, najua Ndio Siasa na mambo ya Utawala, mambo ya mbugani ndio yako hivyo, tuchague Kula au kuliwa.

Kama ushauri wangu utapuuziwa, ni hakika tumeamua kulana wenyewe Kwa wenyewe Kama Samaki huko baharini, utitiri wa Kodi mpaka zisizo na maana yoyote zitaendelea kuibuliwa mpaka watu wakuone,
Too zaidi zitabuniwa ili kunyonya na kunyongana hasa Wale wasio na uwezo.

Zingatia, hata Kodi tutoe watu wote nchi nzima, kanuni ya Kulana nyama inasema; Mliwa nyama kamwe hapaswi Kula nyama yake.
Yaani watu hata wakamuliwe Kodi mpaka wazimie bado hawatafaidi matunda ya Kodi zao.

Kodi wanatakiwa watoe watu wazalishaji, kusema kigezo kiwe umri ni kichekesho 😀😀 cha Wala nyama ambao wanasema Kuku akifikisha umri wa kutaga sharti atage bila kujali wamempa chakula au hawanampa, wamempandisha jogoo au lash! Kinachotakiaa ni mayai.

Ni Sawa na Mungu adai Zaka na Sadaka Kwa mtu ambaye hajambariki chochote kwenye uzalishaji huo ni Uhuni.

Vijana wa sasa wanapitia kipindi kigumu alafu Badala ya serikali kujipanga namna ya kuwasaidia Yoo inapanga namna ya kuwala nyama,

Tusipovamia mataifa mengine;
Tutakulana nyama
Tutanyongana!
Tutageuzana Mishikaki
Tutapigana RISASI na Mikuki
Tutatekana na kufungana
Tutaitana wachawi na walozi,
Tutanyonyana Damu.

Wawekezaji ni muhimu lakini sio muhimu kama Sisi tukiwa wawekezaji zaidi ya wageni.
Serikali inashindwaje kutengeneza matajiri wazawa kuwa wawekezaji wakubwa mpaka tutegemee mataifa mengine kuja kuwekeza hapa.

Taikon anauhakika kuwa wapo watu wenzetu waliotunyonya Damu ambao wanamapesa mengi sana, Kwa nini serikali isiwajengee mazingira ya kuwekeza hapa ndani Kama wameshindwa kuwafunga Jela.

Kuvamiwa na wageni na kugeuzwa vibaraka, machawa na wakimbiza upepo wao ni Jambo linalofedhehesha,
Usalama wa taifa sharti ujue na uwe na moyo wa kizalendo sio tuu kulinda Amani ya nchi lakini pia kulinda maslahi ya nchi Kwa kuhakikisha kuwa Wageni hawatuvamii na kututawala.

Usalama WA taifa mtanijibu Mimi ndugu yenu; Nchi yetu Yale makampuni Makubwa, viwanda na matajiri wakubwa je ni watu wa nchi yetu au ndio tumevamiwa?

Sifurahishwi na kinachoendelea Kwa kweli, hakuna Jambo linaloniumaga na kuliona Kama laana, Kama kutawaliwa na mtu Mgeni, hata mkisema Mimi ni Mbaguzi wala hamtakuwa mmekosea, Mimi siogopi kubaguliwa nikiwa ugenini iweje nisiwe mbaguzi nikiwa nyumbani.

Hizo kodi bunifu na tozo umizi ni Kwa hawa vijana wanaolipwa 150,000 Kwa mwezi na kufanya kazi masaa yasiyopungua kumi na mbili, embu acheni utani.

Hizi Kodi ndio zipo Kwa ajili ya hawa house Girl na houseboy wanaolipwa elfu 50 come on!
Au ndio hawa Bodaboda au hawa Vijana wanaoranda Randa mitaani kubeti bila kazi ya maana?
Au ndio hawa wanawake kutwa kucha ninaowaona wakiombewa Kwa Manabii wa upako?

Kama mkinisikiliza basi tunaweza Anza na masuala Yafuatayo;
1. Boresheni Mazingira ya Kilimo yawe nafuu.
√ Toa mikopo,
√ Ondoa Kodi ya pembejeo, viwatilifu, na zana zote za kilimo.
√ Sambaza maafisa ugavi kila pembe ya nchi watoe elimu Kwa Wakulima.
√ Tengeneza mazingira ya njaa Kwa nchi tunazozimudu, iwe Kwa vita, au Kwa kutoa mazao yenye BEI nafuu ili mazao yetu yanunuliwe Kwa wingi kutokana na Wakulima kuzalisha Sana.

2. Ondoa upuuzi na watu wapuuzi kwenye Media.
Serikali izuie watu wenye akili ndogo kuonyeshwa kwenye media, na upuuzi wao.
Vijana tangu wakiwa wadogo waone mambo ya maana kwenye Vyombo vya habari, sio masuala ya kitoto toto na mambo Rahisi.
Hii itawafanya wasiwe na akili za kipuuzi puuzi.
Nikisema kuvamia tunavamia kiukweli kweli, na tunahitaji Vijana wenye akili za kutosha na wanaojua nini wanafanya.

Sio Vijana ambao hata ukiwapa kazi wanawaza mambo ya kipuuzi yanayofanywa na wapuuzi kwenye media.

Nilitembelea baadhi ya vyuo vya Kati na vyuo vikuu, nikashangazwa na Wanafunzi tena wengine WA masomo ya Udaktari wakiwa na mawazo na mtazamo Kama vile Waigizaji wa mambo ya upuuzi upuuzi tuu! Hii ni kutokana na kile wakionacho kwenye Vyombo vya habari.

Najaribu kusema upuuzi ndani ya nchi Kama unaofanywa na Wasanii sijui Kick sijui upupu gani ufanyike mara moja Kwa wiki iwe sehemu Kama ya vichekesho na jamii hasa Vijana wavichukulie Kama vituko na vichekesho, sio kila siku upuuzi tuu na vituko mwishowe Vijana wadogo watafikiri hayo ndio Maisha, nao tutakuwa na taifa la vituko, vichekesho na upuuzi tuu.

3. Vijana wafundishwe kuthamini wenyeji kuliko wageni.
Ni aibu na kujidhalilisha kumthamini Mgeni kuliko mwenyeji, ni Dalili ya kujiona Duni.
Sio ajabu Rais wetu hata akienda nchi za wenzetu usishangae hapewi mapokezi yanayomstahili, kumaanisha wanatudharau.
Lakini huku kwetu akija Rais yeyote hata Kwa mambo yake binafsi tunamshobokea.
Hili ni tatizo hata kwenye mazingira ya kazi, iwe ni polisi, marafiki, waalimu, madaktari n.k.
Mzungu au muarabu au mhindi akifika anapewa Huduma nzuri kuliko muafrika mwenzetu. Hiyo ni Akili za kitumwa.

Jambo Hilo linaanzia kwenye familia, wazazi tunaowajibu WA kuwafundisha watoto Jambo hili. Mwenyeji ni Bora kuliko Mgeni.

4. Nishati ya umeme isambazwe kila Nyumba
Usiseme pesa tutatoa wapi, huo ni ujanja ujanja. Kama pesa za kuiba zinapatikana ni upuuzi kuuliza pesa za kusambaza umeme zitapatikanaje na wapi.

5. Kusambaza Maji kila kijiji na kila nyumba.

Nimechoka! Acha nipumzike Sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Haki inaenda na wajibu..

Serikali imekuja na mambo lukuki ya kuwainua kiuchumi vijana na moja kubwa ni kwenye sekta ya kilimo na Uvuvi..

Itanunua zaidi ya boti 250 za Uvuvi kwa ajili ya vijana..

Itaanzisha mashamba yaani block farming na kuwawekea miundombinu ya umwagiliaji Ili wazalishe..

Itawapa mikopo ya fedha na zana za kilimo,ufugaji na Uvuvi..

Umesikia itaanzisha mashamba ya kunenepesha mifugo kwa ajili ya nyama na kuuza. Nje,vijana ndio watawekwa kufanya Kazi hizo..

Na mbinu zingine nyingi kwa ajili hiyo,kwa hiyo sio sawa kusema eti vijana wanapitia kipindi kigumu..

Mwisho wakiiongiza kipato lazima walipe Kodi.
 
Mwigulu ni mshenzi sana, hajazungumzia kuhusu serikali kununua ma vi 8 kwa bei mbaya huku kuna aist za bei poa ambapo wanaweza kuokoa fedha za walala hoi kwa kununua gari za kawaida tu.

Jomba kaja na wazo mbadala "waliofikisha miaka 18 walipe kodi"
Damn you Mwigulu 😏
 
Bora punda afe ila mzigo ufike, kodi ni wajibu wa kila raia….. sio kulialia na huduma mnataka.

Majukumu huleta nidhamu, wajibu huleta kujituma…. kijana akijua anapaswa kulipa kodi ni lazima atapambana ili apate.

Dezo dezo huleta udumavu na uduanzi wa akili.
 
Hilo sijakataa ninachokataa ni kulana nyama Kama wachawi.

Tuvamie mataifa mengine
 
Back
Top Bottom