Kodi katika shughuli za kilimo

Joined
Jan 8, 2019
Posts
6
Reaction score
11
Habari za zenu!
Napenda leo kushea makala hii ndogo niliyoiandaa inayozungumzia masuala ya ulipaji wa kodi katika shughuli za kilimo. Na nimeona niilete makala hii hususani katika jukwaa letu pendwa la kilimo, ufugaji na uvuvi kwani kuna baadhi yetu tunaamini hatustahiki kulipa kodi kutokana na shughuli hizi za kilimo na ufugaji

1. UTANGULIZI
Makala hii fupi inaangazia masuala ya utozwaji wa kodi kutokana na shughuli za kodi kwa mujibu wa sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thanani (VAT), Kodi ya Mapato na Sheria ya Ushuru wa Forodha.

2. KILIMO NI NINI?
Kilimo ni shughuli inayomhusisha mtu/taasisi/kampuni ktk shamba kuanzia kununua, kulima, kupalilia, kuweka dawa, kuvuna, kutunza, kusafirisha na kuuza mazao yaliyopatikana katika shamba pamoja na ahughuli za ufugaji na uvuvi

3. MSAMAHA WA KODI KATIKA KILIMO
Ni kweli kuna msamaha wa kodi ya Ongezeko la thamani (VAT) na ushuru wa forodha ila katika vitu kama mbolea na madawa ya kilimo, matrekta kwa ajiki ya kilimo, mashine za kupandia, kuvunia na kupalilia mazao, vifaa vya kunyunyizia dawa, vifaa vinavyotumika ktk kilimo cha bustani, mabanda, majosho nk

Kwa hy bhasi hivi vifaa vinapotumika kuzalishia ktk shughuli za kilimo huleta mapato. Mapato ya kilimo yamegawanyika sehemu mbili.

A. Mapato ambayo mkulima hastahiki kulipa kodi
Haya ni mapato ya wakulima wadogo wadogo ambao wanatumia mavuno ya kilimo kwa ajili ya kujikimu ie subsistence farmers. Mapato yao hayazidi mil 4 kwa mwaka

B. Mapato ambayo mkulima anastahiki kulipa kodi
Hii inawahusu wakulima wakubwa ambao mapato yao yanazidi mil 4 kwa mwaka. Hawa wanastahiki kulipa kodi kulingana na sheria ya kodi ya mapato kama ilivyoainishwa ktk jedwali la kwanza la sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004

4. UWASILISHAJI WA RITANI ZA MAPATO
Mfanyabiashara wa mazao kama mfanyabiashara yoyote mwingine anastahili kulipa kodi ya kutokana na faida ya biashara yake. Hivyo anapaswa kuwasilisha ritani na hesabu za biashara yake

5. MUDA WA UWASILISHAJI MAKISIO YA KODI ie provisional tax
Kwa mujibu wa sheria mkulima anaefanya shughuli za kilimo cha msimu na hafanyi biashara nyingine malipo ya awamu ya kwanza na ya pili hayatakuwepo. Lkn atapaswa kuwasilisha makisio ya kodi ya mapato yake mnamo au kabla ya mwisho wa mwezi wa tisa (Septemba) ya mwaka wake wa mapato. Hii ina maana kuwa atalipa kodi ya awali ie makadirio ktk mikupuo miwili ya Septemba na Disemba

6. UKOKOTOAJI WA GHARAMA ZINAZOKUBALIKA KISHERIA
Si kila gharama inakubalika katika ukokotoaji wa kuandaa mahesabu ili kujua faida halisi itokanayo na kilimo. Gharama za matumizi zinazokubalika ni pamoja na
1. Matumizi yanayolenfa ktk kuendeleza biashara eg pango, umeme, usafirishaji, mishahara etc
2. Punguzo linalotokana na uchakavu wa vifaa na mitambo inayotumika ktk kilimo kwa 100% ya thamani yk ya mwaka wa kwanza toka kununua (rejea jedwali la 3 la shearia ya kodi)
3. Gharama za utafiti, uboreshaji, utunzaji mazingira za kilimo etc
4. Gharama nyinginezo ambazo kamishna wa kodi ataridhia lkn zikiwa na lengo la kuendeleza kilimo

7. UTOZWAJI WA KODI KWA VIFAA VYA KILIMO TOKA NJE YA NCHI
Uingizaji wa vifaa vya kilimo hautozwi ushuru wa forodha na pia VAT haitatozwa kwa vitu kama mbolea, madawa na mazao ya kilimo ambayo hayajasindikwa.
Hata katika uuzaji wa mazao ya kilimo hakuna ushuru wa forodha na bidhaa isipokuwa korosho zisizobanguliwa na ngozi ghafi. Zingatio liwe si kwa mazao yaliyopigwa marufuku

8. USAJILI WA ONGEZEKONLA THAMANI-VAT KWA MFANYABIASHARA YA MAZAO
Endapo mfanyabiashara huyu anashughulika na vifaa vya kilimo pekee HASTAHILI kusajiliwa VAT hata kama mauzo yake kwa mwaka yanazidi mil 100.

Lakini endapo mfanyabiashara huyu anashughulika pia na kuuza bidhaa zinazostahili kutozwa VAT na mauzo yk yanafika zaidi ya mil 100 anastahili na anakidhi vigezo vya kusajiliwa VAT. kusajiliwa kwake kutatokana na mauzo yake ya biadhaa zinazotozwa kodi na atapaswa kutumia njia sahihi ili kutambua kodi sahihi ya VAT ktk manunuzi anayostahili kujirejeshea

9. ULIPAJI WA KODI KWA KUUZA SHAMBA
Mkulima mkubwa mwenye shamba atatkiwa kulipa kodi itokanayo na mauzo ya rasilimali ie capital gain tax ya 10% ya tofauti kati ya gharama zake ktk shamba hilo na bei halisi aliouza rasilimali hy.

Kodi haitatozwa endapo mauzo ya shamba hilo ni pungufu ya sh mil 10na shamba hilo limetumika kwa shughuli za kilimo kwa angalau miaka miwili kati ya miaka mitatu kabla ya kuliuza.

Pia unatakiwa kulipa ushuru wa stemp ambao ni sh 500 kwa heka ili kuhalalisha uhamishaji wa umiliki wa shamba hilo kutoka kwa muuzaji kwenda kwa mnunuzi.

10. KUKATA RUFAA
Iwapo mfanyabiashara wa mazao hajaridhika na makadirio aliyoandikiwa anayo nafasi ya kukata rufaa ndani ya siku 30 baada ya kupokea makadirio. Rufaa yake atawasilisha ktk ofisi ile ile aliyokadiriwa makadirio akiambatanisha na vielelezo vyote ambavyo vitasaidia ktk kutoa maamuzi sahihi

Asanteni sana!
(mniwie radhi, kiambatanisho cha kodi ktk majedwali kinagoma kukaa ie attached, kikikubali mtaona hapo)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…