Kodi kwenye youtube,instagram na tweeter bussness account

Luqman mohamedy

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
899
Reaction score
1,231
Bussness account(akaunti za biashara) ni akaunti ya kawaida kabisa kama nyingine inayotumia jina"brand" ya biashara fulani.

Zinaweza kuwa pia akaunti binafsi za watu maarufu na za watu wenye idadi kubwa ya mafollowers na viewers zinazotumika kutangaza matangazo ya biashara kwa malipo.

Wamiliki wa account hizi kwenye nchi zilizoendelea kama US wanahesabiwa kama watu WALIOJIAJIRI(selfemployed) na wanalazimika kulipa kodi "self-employment tax" pale wanapoingiza mkwanja kupitia account zao 'pay-as- u earn'.

Kwa wale wenye account hizi facebook na instagram nk itawalazimu wao na makampuni waliyoingia ubia nayo walipe kodi kulingana na thamani ya tangazo lao ambayo pia inategemeana na thamani ya mwenye account na idadi ya followers.


Mfano Lebron James anaingiza mpaka Mil 80 akipost tangazo moja kwenye account yake binafsi ya instagram huku Cristiano Ronaldo,Messi na Neymar Jr wanaingiza mpaka mil 110 kwa kupost tangazo moja kwenye account zao binafsi za mitandao ya kijamii na inawalazimu kulipa mpaka kodi ya 20% kwa kiasi walichoingiza.

Sasa kama utaweza kuwalipisha kodi wamiliki wa blog na account za youtube(hapa inajumuisha hizo wanazoita online TV) za biashara kulingana na matangazo,idadi ya viewers na idadi ya walioperuzi(kiasi cha megabytes alizoingiza) na malipo kutoka youtube headquater unapaswa uwalipishe na wanaopost matangazo ya biashara kwa malipo kwenye instagram na other social network kwa kuwa baadhi yao wanapata pesa mpaka mara 30 ya muuza matunda anayeuza sokoni na analipa ushuru kama kodi yake kwa kazi anayoifanya toka alfajiri mpaka magharibi.Otherwise wasipolipa labda tuwaite MACHINGA WA MITANDAONI maana machinga ndio hawalipi kodi.
 
Luqman mohamedy ina maana mimi nichapwe kodi (let say 10%) kukupa tangazo langu. Then wewe uchapwe (letsay 15%) kuliweka mtandaoni!?..
Hii itakuwa sio aina mpya ya double taxation!?..
 
Luqman mohamedy ina maana mimi nichapwe kodi (let say 10%) kukupa tangazo langu. Then wewe uchapwe (letsay 15%) kuliweka mtandaoni!?..
Hii itakuwa sio aina mpya ya double taxation!?..
Let say If tax ni 20% na unalipisha tangazo moja 10000 then utatoa 5000 ambapo mlipaji(mwenye tangazo) atakuwa katoa indirectly na wewe uliyelipa(mwenye kupost) directly.Kodi analipa aliyefanya biashara sio aliyeomba kutangaziwa
 
Sielewi sana hapo lakin mwanzo nilikuwa nalipia matangazo kwa wasanii wakubwa mpaka laki moja Kwa wiki....siku nilifunguka kuna Ku kulipia Na kadi yangu ya bank kwa Mr Fb imeniokoa sana mana kwa dollar hata 2 kwa siku unauza poa tu
 
kodi ni muhimu kwa kila kipato unachopata. Lakini hao wakina Neymar na Lebron husajili hizo account zao au hupeleka taarifa ya kipato chao cha mwaka kwa mamlaka za kodi?
 
kodi ni muhimu kwa kila kipato unachopata. Lakini hao wakina Neymar na Lebron husajili hizo account zao au hupeleka taarifa ya kipato chao cha mwaka kwa mamlaka za kodi?
Wana watu wao wa social media, accountants, public speakers so wapo vizuri mkuu, LeBron James ni km taasisi mkuu, kila kitu anachofanya kinaangaliwa na dunia
 
Let say If tax ni 20% na unalipisha tangazo moja 10000 then utatoa 5000 ambapo mlipaji(mwenye tangazo) atakuwa katoa indirectly na wewe uliyelipa(mwenye kupost) directly.Kodi analipa aliyefanya biashara sio aliyeomba kutangaziwa
Lakini si unajua hiyo sio biashara ya kampuni ambayo inatozwa kwa awamu so atakayetozwa ni End-Consumer!?.. Nashauri jifunze mambo ya VAT mkuu!.
Halafu kifaa chochote unachonunua kina kodi 18% ambayo ni kubwaa!. Sasa ikiwekwa 20% si tutakufa boss!..
Kwa mfano; 10,000 kodi yake (18%) ni 1,800/= so ukipewa Tangazo la bei hiyo ina maana tayari 1,800 ya TRA hiyo 8,200 ni yako!..
Au sijakuelewa!?
 
Wana watu wao wa social media, accountants, public speakers so wapo vizuri mkuu, LeBron James ni km taasisi mkuu, kila kitu anachofanya kinaangaliwa na dunia
Kwenye kodi kuangaliwa na dunia hakujalishi.
wale hawajasajiri mamlaka ila wanapeleka taarifa zao za kibank na biashara then zinakatwa kodi directly!..
 
Luqman mohamedy ina maana mimi nichapwe kodi (let say 10%) kukupa tangazo langu. Then wewe uchapwe (letsay 15%) kuliweka mtandaoni!?..
Hii itakuwa sio aina mpya ya double taxation!?..
Itakua kama tax ya Uganda social media tax wao wanaita over the top tax(OTT).yaani watu wanawaza vitu vya kijinga sana mkuu!badala ya kuwaza Na namna ya kuboresha mazingira ya kusupport serial entrepreneur.. MTU anakuja Na wazo kama hili...bado sana tz
 
Umeshabet?kuna kampuni tax 20%..jarbu kama unabet then soma mkeka
 
Mkuu upo nyuma sana kama hufahamu commnctn sectr ndio inaongza kwa kulipa ukiacha huo ujasiria mali wako.Bill gate na Mark Zukerberg hawatengenezi sabuni wala kulima.Kuna watu wanaishi kwa hizo social ntwrk we endelea kuwaza ufugajinawa sato wakati simu unayo kiganjani inakutajirisha
 
Nguvu kama hizi zingetumika kwa kina Jeff Bezos leo hii wangebaki kuzoa taka tu!. Cheki Jack Ma anavyojaribu kuwasaidia wajasiriamali wadogo kupitia Alibaba!.
Social Media zenyewe kwa bongo hazijakuwa kuanza banana hivi!.
 
Umeshabet?kuna kampuni tax 20%..jarbu kama unabet then soma mkeka
Ukinunua pen ya sh. 200 tambua ndani yake ina kodi ya 18%, ukinunua shati la 25,000 ndani yake lina 18%, ukinunua simu ndani yake ina 18%.
Kampuni za kubet zimeongezwa kodi kuanzia mwaka huu wa kodi ilikuwa 18%. Lakini tuulizane wangapi wanafanya hiyo michezo!?.
Halafu tambua kupandisha kodi au kupunguza kodi ni matokeo ya kuamua kudiscourage matumizi ya vitu fulani au kuencourage matumizi ya vitu fulani!. Mpaka leo hii 18% tunailalamikia ni kubwa na inatuumiza tukiomba ishuke!.
Kuna vitu kama Chakula na Mazao, Mashule, Vifaa vya kilimo na Pembejeo hayana kodi haya hii yote ni ili kusaidia/kuencourage matumizi yake zaidi!.
Ukiangalia sijui kampuni la kubet linachapwa kodi 20% kwa mkeka basi na kodi ya Kununua Simu au kifaa iwekwe 20% nasikitika hujajua Impact yake!..
Kubet ni ujinga unaokuwa kwa kasi inabidi kuupunguza kwa kuuongezea kodi!.
 
Unaongelea Tanzania hii!??... Unaweza itetea hoja yako boss!?.
 
mkuu hujanielewa,nachosema kwanini mtu anawaza kuweka kodi kwenye social media?huoni kua unanyima watu fursa ya kujingiza kipato..ndo maana nikasema watu wanawaza makodi ya kijinga.....
 
Watu mnawaza ujinga tu,umepata faida gani kwa wazo lako hili la kijinga,hebu fikiria ulipe kodi kwenye vocha,ulipe ya kununua simu na ulipe ya social media,Bongo secta ya mitandao ya kijamii haijakuwa kubwa mpaka kufikia kulipishwa kodi namna hiyo,hata hao mabloger wanaonewa tu,wabongo waliojiunga na social media hawafiki hata 5milion,na Active user hawafiki hata millioni 3 halafu unataka kodi unafikiri kwa kutumia kiungo gani?,bila shaka wwe utakawa chama cha mbogamboga umenikera kweli wwe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…