Kodi Mpya kwenye Bajeti Mpya

Kodi Mpya kwenye Bajeti Mpya

hekimatele

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2011
Posts
9,890
Reaction score
2,795
Wadau katika pita pita zangu nimekuwa nikisikia juu ya ongezeko la kodi kwenye maeneo mbalimbali ya uchumi.
Aidha watu wengi wamekuwa wakilalamika juu ya ongezeko la kodi kwenye vinywaji vya kileo.
Leo nimekutana na mfanyabiashara mmoja analalamika kuhusu ongezeko la kodi. Anaendesha biashara ya Pub ambapo anauza vinywaji.
Awali anadai alikuwa analipa hadi mpaka 360,000/- kwa mwezi ikiwa ni kodi ya mapato. Kwa mujibu wa bajeti hii mpya ambayo itaanza kutumika rasmi kuanzia Julai watatakiwa kulipa asilimia 100 juu yake. Kwa ufupi atatakiwa kulipa 720,000/- kwa mwezi.
Ukija kwenye uhalisia, wakati analipa kodi ya mwanzo alikuwa anasuasua kwa sababu biashara yake ina msimu. Kuna msimu ambao kwa siku anauza mpaka bia chupa 5 tu, na kuna msimu anauza mpaka kreti 3 kwa siku.
Sasa hivi anafikiria kufunga biashara yenyewe kwa sababu haitamlipa.
Swali langu kwa TRA, wamefikiria nini mpaka kuongeza hiyo kodi katika kiwango hicho?
Hawaoni kuwa watapoteza pato kubwa badala ya kuongeza? Na pia kuongeza mianya mingi sana ya wafanyabiashara wengi kukwepa kodi?
Kuongeza kodi kwa bidhaa za ndani ndio njia pekee ya kuongeza pato la ndani? Na je hawaangalii athari zinazotokana na ongezeko Hilo?
Karibuni tuchangie kwa pamoja great thinkers manake athari zimeshaanza kujitokeza kwenye uchumi ambapo mwishowe itasababisha more unemployment and leading to crimes in the country.
 
Hawa tra wana vichwa maji,wao wanachowaza ni kumkandamiza mwananchi tu hawafikirii kukusanya kodi kwenye migodi na utalii.
 
Mkuu, tra wanajuaje kuwa kuna wakati anauza chupa 5 na wakati mwingine kreti tatu?
Kuna rekodi yoyote inayoonyesha hayo?
Kama hakuna ni vigumu kumkadiria kodi.
 
Mkuu, tra wanajuaje kuwa kuna wakati anauza chupa 5 na wakati mwingine kreti tatu?
Kuna rekodi yoyote inayoonyesha hayo?
Kama hakuna ni vigumu kumkadiria kodi.

Huo ni mfano tu ambao jamaa ameutoa,lkn kiukweli wananchi wa Tz tutazidi kugaragazwa na sijui km tutafika!,km tutafika basi tutafika tukiwa tumechoka sana!!!.
 
Yaani nchi hii hovyo sana,hebu fikiri vyanzo vya kiuchumi vya nchi hii vilivyo vingi;tuna migodi ya dhahabu,Almasi,Tanzanite ,Uranium,Makaa ya mawe;Tuna Mbuga za wanyama,Tuna Bahari,Maziwa na mito mikubwa;Tuna gesi,utaliii,majengo,Ardhi,n.k.sasa je Serikali inashindwaje kutumia vyanzo hivyo kujiongezea mapato?,kuliko kubanana na vinywaji jamii ya pombe na sigara.Jamani yaani wanatushinda hata nchi ndogo km Rwanda hata Burundi,sasa Wa-tz tunakuwa Kubwa jinga.
 
Back
Top Bottom