Haipo hivyo, kwanza gari ambayo ilikuwa exempted h
uwa ina depreciation value, mathalani wakati inaingia cif value yake ilikuwa ni milioni 10 basi utapiga asilimia kama 60 hivi kwa gari iliyoingia mwaka huo 2012 yaani 10,000,000*60% unayopata mil 6 then unachukua mil 10 toa 6 unayopata 4mil ndio inakuwa current CIF, ambayo uta calculate kodi from that 4mil. Ndio maana hao wamemwambia apaleke doc wakati gari inaingia ili ijulikane thamani yake ilkuwa kiasi gani, lau kama ikishindikana ni lazima aende toyota tanzania wampe kalatasi ya valuation ya kuonesha thamani ya gari kipindi hicho ilikuwa shingapi? Ila kwa kusema tu mil 50 bila ushahidi utajiumiza mwenyewe tu maana kipindi hicho gari hyo ilikuwa dola haizidi 25,000 ambapo pia dola ilikuwa chini. Kwamfano tuchukue hiyo milioni yake 50 uki depreciate kwa hiyo miaka ni kama 70% thamani ya gari ya sasa inaweza kuwa mil 15 hapo ndio utapiga kodi. Ila lazima apeleke docs ili afanyiwe fair assessment.
Na pia gari aliingiza nani?
Kama ni mfanyakazi maana yake alisamehewa vat tu hivyo atalipa importy duty, ex duty ya cc na other charges
Ila kama ni shirika au returning hakulipa chochote hivyo utalipa kodi zote. Huo ni uzoefu mdogo nilionao maana tuliwahi kufanya gari kama hilo la jamaa yetu