Inapotokea unapokopa kwenye mabenki yetu kama mfanyabiashara au mfanyakazi, hesabu zinaonyesha utarudisha kati ya asilimia 40 - 60 zaidi ya kile ulichokopa. Percentage hii inategemea muda wa kulipa. Nataka wenye utaalamu watueleze sheia ya fedha inasemaje juu ya asilimia ya jumla atakayorejesha mkopaji baada ya kuchukua kiasi fulani cha fedha? Je sheria iko kimya hivyo kuyapa mabenki kufanya maamuzi kwa kadri wanavyojisikia? Naomba tuliweke hili wazi ili liweze kuamsha majadiliano na pengine mabadiliko. Na hii inaweza pia kuleta changamoto wakati huu ambao tunafikiria kuwa na morgage act. Kwa nchi za wenzetu (zilizoendelea) riba wakati mwingine haifiki hata 5%.
Cha ajabu ni kuwa, wakati mabenki yakiendelea kutangaza kupata faida, bado yamekuwa yakiongeza riba, gharama za ATM withdraw, transfer, deposit, nk.