Kodi za mabango ya biashara zikoje?

Kodi za mabango ya biashara zikoje?

cliff

Member
Joined
Feb 7, 2008
Posts
21
Reaction score
32
Miye ni mjasirialmali mwenye hamu ya kujikwamua kiuchumi. Naomba kujua yafuatayo kuhusu kodi ya mabango ya matangazo ya biashara:

1. Ukiweka bango kwenye Barababa, kwa mfano ya Sirari - Mwanza linatozwa kodi na TARURA au na TANROADS? Nauliza kuhusu hizi taasisi mbili kwa vile inavyoelekea hili jukumu limeondolewa kwenye kwenye TRA(?).

2. Viwango vikoje kwa mfano kwa bango la 100x200cm?

3. Viwango hivi vimechapishwa/vimetangazwa mahali tupate links?

4. Je, ukiweka nje ya hifadhi ya barabara (yaani ndani ya eneo la kiwanja chako) napo unadaiwa kulilipia? Kiwango kikoje au ni kama hicho cha juu?

Natanguliza shukurani.
 
Mamlaka husika ndo wanajua , tozo hzo hazipo online so ni manual, kuna bara bara zinasimamiwa na Tanroad na zingine Tarura, kila mmoja anatoza panapomhusu , hakuna tozo Kwa bango lililo nje ya hifadhi ya bara bara.....au nasema uongo ndugu zangu
 
Kodi za mabando zinasimamiwa na TRA.Nafikri ni kati ya 18000 hadi 25000 kwa sf. kwa mwaka
 
Mzee...kuwa makini hao tra hawafai..hapa khm wanapita mtaani na tape wanapima bango wanakuandikia samasi mkajadiliane ulipe kuna dogo mmoja aliweka akaambiwa ni laki nne walipoenda kwenye vipimo na hesabu ikawa laki mbili na upuuzi hio ni bango tu kwa mwaka bdo hujaladiriwa bado ile nini wanaita..withholding tax ya mwenye nyumba..shabashi lazima ukae..
 
Back
Top Bottom