Kodi za nyumba Dar es Salaam kuwa juu

junior rookie

New Member
Joined
Dec 19, 2024
Posts
1
Reaction score
3
Hivi nini kinapelekea bei za kodi za nyumba dar es salaam kupanda sana na ghafla? Yani vipato havipandi ila bei za kodi za nyumba ni ghali sana na mnoo serikali inabidi iliangalie ili suala na liingilie kati. Yani mfano nyumba sinza chumba master, forced jiko ni laki nne kweli?

 
kipindi nikiwa kwa remi-sinza nilikuwa naona madalali wakija lazima utoe hela ya kuonyeshwa chumba/nyumba na hapo ni 2020

Ila Kigamboni sijaona utaratibu wa kumlipa dalali ela ya kuonyeshwa room..
 
Kodi inategemea na eneo ubora na hadhi yake n.k, nyumba yenye kigezo kama hiko na si ajabu ikawa hivyo kila kitu ukiikuta Chanika ama mpiji magoe utashangaa bei inashuka hata nusu yake

Cha msingi kama unajitafuta ni bora uanzie nje ya mji lakini katikati ni mtihani kwa kweli unaweza shangaa kibanda tu

Bei ya kufa mtu
 
Kama wewe siyo Mgeni nchi hii, Sioni ulazima kuishi Sinza.
 
Wenye Nyumba wanalia kwamba bei zimeshuka baada ya serikali Kuu Kuhamia Dodoma.Bei ya 400K Kwa Sinza bado ipo chini.Hizo ni bei za Kimara au Kinyerezi huko.Maeneo mengi ya Dar Siyo rafiki Kwa Uwekezaji wa Nyumba za Makazi Kwa sasa ukilinganisha na gharama za Uwekezaji.Jiulize Ardhi ya Sinza Kiwanja cha SQM 300 Kwa sasa ni bei gani.Ndiyo maana wengi Wabadili Nyumba zao kuwa AirBnB,angalau Malipo ya Kila siku yanatosha kufidia gharama kubwa za Uwekezaji.Piga hesabu Ununue Kiwanja na ujenge na utarajie marejesho ya Fedha angalau Miaka 6.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…