Pasco_jr_ngumi
JF-Expert Member
- Nov 20, 2010
- 1,802
- 283
Koffi Olomide, ambaye ni mwanamuziki mashuhuri
barani Afrika ameshitakiwa kwa kumpiga
Mtayarishaji wake wa muziki. Mwanamuziki huyo alikamatwa na kufungiwa katika
kituo cha polisi na kufikishwa mahakamani
jumatano. Koffi alikamatwa kufuatia vurugu katika hoteli moja
mjini Kinshasa. Waandishi wa habari wanasema mahakama hiyo ya
Kinishasa ilifurika kutokana na watu wengi kuja
kumuona kiongozi huyo wa bendi ya Quartier Latin
akiwa kizimbani. Kesi hiyo iliharishwa hadi Alhamisi asubuhi wakati
atakaposhitakiwa rasmi. Wakati wa kesi hiyo hapo jana Koffi Olomide
aliwakilishwa na mawakili 10. Ugomvi kati ya mwanamuziki huyo na mtayarishi
wake Bwana , Diego Lubaki, ni kuhusu pesa dola
$3,680. Hakimu alimfahamisha mwanamuziki huyo ikiwa
atapatikana na hatia huenda akafungwa jela miezi
sita. Olomide ni gwiji wa muziki aina ya "soukous",
mtindo ulitokana na jina la kifaransa "secouer", lenye
maana ya kujitikisa au kujinengua ,na wachezaji
wake vile vile wanatambulika kwa kunengua
maungo.
Source. bbc swahili