Koffi Olomide ndio msanii bora wa muda wote kutoka Congo

Kibundi wa getto

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2013
Posts
455
Reaction score
877
Leo acha niseme ukweli wakuu,watu wanapenda kutompa mtu sifa zake mpaka afe.
Toka kizazi cha kina Lwambo mpaka sasa kina ferre na fally hakuna msanii wa kumlinganisha na koffi kimuziki apo Congo.Sema watu wanapenda kutukuza vitu vya kale kama kwenye mpira wanavyompaisha Pele na Maradonna wakati messi na Ronaldo wamefanya mengi makubwa tu.

Sasa basi hata kwenye mziki,utasikia sijui Madilu,Papa wemba sijui nani.Ndio wametoa nyimbo kali sana lakini hakuna aliefanya consistency ya nyimbo nyingi kuwa juu kama koffi.
Hata huyo Werrason bado anapaishwa tu kwa nyimbo chache ukifananisha na Koffi.

Tukubali tu wakuu hakuna kama Koffi kwenye muziki wa boringo.
 
Mimi huwa nikisikia huu wimbo wa Koffi olomide-Loi aisee nitakurupuka hatakama nilikuwa bafuni,huu wimbo huwa unanibamba sana,

Mwanzoni mwa video ya loi manati kubwa inavutwaaaa sanaa.

Hili jamaa inaonekana gemu limelihimili toka miaka na miaka.

Loi.... loi.... loi.... loi.
 
Toka kizazi cha kina Lwambo mpaka sasa kina ferre na fally hakuna msanii wa kumlinganisha na koffi kimuziki apo Congo
Mkuu wewe furahia tu mziki wa Koffi. Kwa sisi wa enzi hizo tunajua huwezi kuwaweka chungu kimoja hao ulio wataja na Luambo. Franco Luambo Makiadi ni habari nyingine kabisa-ukiongelea muziki wake unaongelea muziki wa TP OK Jazz huenda ikawa bendi bora zaidi kutokea CONGO na Africa kwa ujumla. Hiyo ndio bendi ya Vicky Longomba, Poete Lutumba Simaro, Commandant de Bord Josky Kiambikuta, Ntessa Dalienst, Ndombe Pepe, Sam Mangwana, Madilu System, Djo Mpoy, Kiwakana Aime, Checain Lola Djangi kukutajia wachache. Miaka ya 1980 kwa mfano TP OK Jazz ilikuwa na wapiga solo (5) Franco, Papa Noel, Thierry Mantuika Kobi, Gerry Dialungana Kasia, Dizzy Mandeku-sikiliza nyimbo za wakati huo au wasome hao jamaa kwani wote ni who is who kwenye muziki wa Zaire. Luambo ni mwanamuziki wa kwanza kujengewa SANAMU "monument" huko CONGO miaka 26 bada ya kufariki na kufanyiwa international conference ya kujadili muziki wake. Luambo ana kitu inaitwa "OK Jazz School of Music". Kabla ya Tchacho ujuwe kulikuwa na Rhumba Odemba ambayo bado ipo ndani na nje ya Congo. Kuhusu gitaa ya Franco check hii youtube na pia google "Syran Mbenza & Ensemble Rumba Kongo: Immortal Franco: Africa's Unrivalled Guitar Legend" Kuhusu maisha ya Franco check hiki "Congo Colossus: The Life and Legacy of Franco & OK Jazz Paperback – January 4, 1994 by Graeme Ewens (Author)"
Wikipedia wanasema "

François Luambo Luanzo Makiadi (6 July 1938 – 12 October 1989) was a major figure in 20th-century Congolese music, and African music in general. He is widely referred to as Franco Luambo or, simply, Franco. Known for his mastery of rumba, he was nicknamed the "Sorcerer of the Guitar" for his seemingly effortless fluid playing. As a founder of the seminal group OK Jazz, he is counted as one of the originators of the modern Congolese sound." Sikatai Koffi yuko vizuri sana lakini ukimuweka yeye na Luambo ni sawa na mzee Mwinyi alivyosema "Nyerere ni Kilimanjaro na yeye ni kichuguu". Mkuu furahia Tchacho.
 
weka mbali na watoto mzee kofii olomide,, kuna ile inaitwa plus noma sanaa
 
Papaa Mopao,, kiukweli huyu jamaa anastahili sifa zake.
Toka nimeanza kuifahamu albamu yake 'Maggie' na kundi la Quartier Latin enzi nikiwa nimeanza shule ya msingi miaka ya 1995 mpaka leo hii bado jamaa yupo ktk ubora wake ule ule.

Kundi lake la Quartier Latin ambalo liliasisiwa kitambo hicho 1986 limetoa wasanii wengi sn wanaofanya vizuri kama Fally Ipupa, Ferre Golla nk ambao kwa sasa hawapo tena kundini, ila cha kufurahisha zaidi ni ule upendo na ushirikiano wanaoendelea kuoneshana baina yao kwa mfano mwaka 2016 Fally Ipupa aliorganize tamasha la 30th Annivessary ya lililokuwa kundi lao la Quartier Latin wasanii wengi waliopitia kundi hilo akiwemo the founder himself Papaa Mopao alishiriki vizuri sana.

Ila Koffi Olomide Ngoma zake za miaka ya hivi karibuni 'Abracadabra' na 'Danger De Mort' nazikubali sana!!
 
Franco Luambo "grand maitre" utamuweka wapi?
Nitamuweka kundi lile la "Ma-Grand Maitre" ambamo Kalle Jeff Tshamala na Franco Luambo walitunukiwa na wanamuziki wa Zaire May 1980. Grand Kalle kwa kazi ambayo alishafanya (alisha fikia ukingoni kimuziki)"Baba wa Muziki wa Kisasa wa Congo" na Franco kwa yale aliyokuwa akiyafanya (ndiyo Franco na TP OK Jazz walikuwa hawa shikiki kwa ubora wa kazi zao). Wanaoweza kukaribia kundi hili ni Le Poete Simaro Lutumba, Tabou Ley na Vicky Longomba).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…