Koffi Olomide ndio msanii bora wa muda wote kutoka Congo

Jamaa anajitahid sana kumudu mziki wake pia ni mvumilivu katka tathnia yake kutokana na changamoto mbalimbali anazokutana nazo,big up koffi
 
Aah aisee Mimi kwangu ni Pepe kalle na Empire bakuba yake, pembeni yuko Papy Tex...
Kuna vibao vinakonga sana moyo wangu, mfano "kanda ya nini ya Papy Tex,La lumbalumba, Moyibi, Hidaya, Gilant, kaliki
Nyimbo hutumii nguvu nyingi sana, jamaa alikua anajua sema tuu alitangulia mapema mbele za haki
 
sebene lipo?gitaa maana raha ya congo man hata nyimbo ikiwa ya taratibu unacheza kiboss boss hapo ndo koffi alipotuwin
Kwani sebene limeanzia wapi? Kama ni gitaa basi OK Jazz na TP OK Jazz ya Luambo ni habari nyingine kabisa. Shiko Mawatu (Soukus Stars, amepiga sana na Madillu post OK Jazz) anakuambia akiulizwa wapiga solo wakali 3 kushinda wote huko DRC atakuambia ni (1) FRANCO, (2) LUAMBO, (3) MAKIADI hayo yote ni majina ya mtu mmoja. Syran Mbeza (Lovy du Zaire, Kekele, 4 Stars) ametoa album inaitwa Immortal Franco: Africa’s Unrivalled Guitar Legend. Hapo ingiza solo la Papa Noel, Gerry Dialungana,na Bass la Mpudi kionjo cha rythm ya Papa Lutumba, Makoso, unapata kitu Papa Tshimanga Asossa (Negro Success, Lipua Lipua, Kamale, Fuga Fuga, Sikinde, Marquis, Bana Marquis) anakuambia ngoma ya watoto hailali, lazima wakubwa watambe. OK Jazz (1956-1993) haitegemewi kutokea tena. Bingwa wa muziki wa taratibu enzi hizo alikuwa OK Jazz katika mtindo wa BOLERO-ingia Youtube tafuta "suite letter no 1" uonje utamu.
 
Toka dunia iumbwe mpaka sasa hakuna msanii na mwenyekipaji kma kofi olomide akifatiwa na oliver ngoma,mocika seka na chakachaka
 
Koffi Olomide a.k.a
1.Thirteen Apostle
2.Zando ya Munene
3.La Rambo Du Congo
4.Guardiola
5.Barack Obama
6.Mopao Sarkozy
7.Papa Mourinho
8.Favorite Dish
9.Nzambe ya Bana Africa golden ball
10.Mopao Mokonzi
11.Grand Mopao
12.Quadra Kora man
13.Wold no 1
14.Rapid intervention Force
15.Fololo Papa
16.Effrakata
17.Mukulu Kulu
18.Eza Mayi
19.Tcha---Tcho
20.Papa Plus
21.Makila Mabe
 
mmenikumbusha ngoja nidownload mijisong yake
 
Huu ni ukweli. Mopao noma. Ukisikiliza vibao vya Magie, Loi, petit na London, Micko, Ultimatum aaaah utadhani vimefyatuliwa mwezi uliopita. Kofie dunia nyingine, acheni tu.
 
Kwangu Mimi Pepe kalle ni zaidi, ngoma zake zote ni kali, ataimba kiswahili sawa, kingereza au kifaransa sawa tuu, ukija kilingala ndo kabisa,
Yule ni tembo wa Afrika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna ile ngoma inaimbwa...nanga nanga nanga kolelangaaaaa mwana mama aaaah mwana maaaama aaaaah....sijui inaitwaje hiii

Sent using Jamii Forums mobile app
Inaitwa Maggie, ilikuwa ni moja ya hit song iliyofanywa na Koffi Papaa Mopao akishirikiana na kundi lake la Quartier Latin na ndo ilibeba jina la album iliyotoka 1994.

Koffi ni moja ya wasanii ninao wahusudu sana ktk anga za music duniani. Tangu nipo vidudu (nursery) mpaka leo hii nipo kazini huyu mzee bado anatoa pini tu na zote ni moto!!!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anajua sana kuichezea sauti yake, pia anajua kuwapangalia vijana wake, check ngoma kama Respect, Monde arabe, Gilba, Biblia, ........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reactions: tyc
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…