Komamanga huzuia kansa ya matiti isitambae

Komamanga huzuia kansa ya matiti isitambae

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

KOMAMANGA.jpg



Uchunguzi mpya umeonyesha kwamba, katika tunda la komamanga kuna kemikali zinazozuia kansa ya matiti isitambae mwilini.

Uchunguzi huo uliochapishwa katika jarada la Utafiti la kuzuia Kansa umeonyesha kwamba, kemikali ziitwazo ellegitannins zinazopatikana kwa wingi kwenye komamanga, zinaweza kuzuia

kimeng’enyo (enzyme) aina ya aromatase, suala ambalo huzuia kukua kwa Homoni ya estrogen inayopatikana katika kansa ya matiti.

Shiuan Chen Kiongozi wa uchunguzi huo amesema kwamba, kemikali hizo hupunguza uzalishwaji wa estrogen, na kusaidia kuzuia seli za kansa ya matiti zisizaliane mwilini, pamoja na tezi la ugonjwa huo lisikue.

Aromatase, ni kimeng’enyo ambacho hugeuza Homoni ya androgen kuwa estrogen, na kushambulia kimeng’enyo hicho ndio lengo kuu la dawa za kupambana na kansa za matiti zinazosababishwa na homoni ya etrogen.

Huko nyuma pia uchunguzi ulionyesha kwamba tunda la komamanga lina faida kubwa kiafya hasa kwa kuwa na anti Oxidant nyingi na vitamin mbalimbali, ambalo huzifanya tunda hilo

liweze kusaidia katika kupambana na magonjwa ya saratani, matatizo ya moyo na hata ugonjwa wa kusahau uzeeni au Alzheimer.

Anti Oxidant huzuiaradikali huru ambazo ni hatari sana kwa miili yetu. Uwezo huo hupelekea mwili kukabiliana na magonjwa mbalimbali hata ugonjwa wa homa ya mafua ya nguruwe. Kama
huwez
i kupata tunda la komamanga sokoni, basi unaweza kutumia juisi ya Komamanga na daima tutunze afya zetu!

FAIDA YA JUISI YA KOMAMANGA

  1. Huweza kuzuia maendeleo ya saratani ya mapafu.
  2. Hupambana na saratani ya matiti
  3. Hupunguza ukuaji wa saratani ya kibofu
  4. Inaweza kuzuia na kupunguza kasi ya ugonjwa wa Alzheimer
  5. Inapunguza kolesterol
  6. Hushusha shinikizo la damu
  7. Hulinda meno
Inasemekana ukinywa juisi ya komamanga (pomegranate) nusu lita kila siku kwa muda wa mwezi mmoja, inasaidia kupunguza mafuta tumboni kwa wale wenye vitambi. Jitahidi kuwa na matumizi ya haya matunda unufaike na uboreshe afya yako.
 




Uchunguzi mpya umeonyesha kwamba, katika tunda la komamanga kuna kemikali zinazozuia kensa ya matiti isitambae.


Uchunguzi huo uliochapishwa katika jarida la Utafiti wa Kuzuia Kensa umeoneysha kwamba, kemikali ziitwazo ellegitannins zinazopatikna kwa wingi kwenye komamanga, zinaweza kuzuia

kimeng’enya (enzyme) aina ya aromatase, suala ambalo huzuia kukua kwa homoni ya estrogen inayopatikana katika kensa ya matiti.


Shiuan Chen Kiongozi wa uchunguzi huo amesema kwamba, kemikali hizo kupunguza uzalishwaji wa estrogeni, na kusaidia kuzuia seli za kensa ya matiti zisizaliane, pamoaja na tezi la ugonjwa huo lisikue.

Aromatase, ni kimeng’enya ambacho hugeuza homini ya androgeni kuwa estrogeni, na kushambulia kimeng’enya hicho ndio lengo kuu la dawa za kupambana na kensa za matiti inazosababishwa na homoni ya estrogen.

Huko nyuma pia chunguzi zilionyesha kwamba tunda la komamanga lina faida kubwa kiafya hasa kwa kuwa na anti oxidanti nyingi na vitamini mbalimbali, ambazo hulifanya tunda hilo liweze kusaidia katika kupambana na magonjwa ya saratani, matatizo ya moyo na hata ugonjwa wa kusahau uzeeni au Alzheimer.


Anti oxidanti huzuia radikali huru ambazo ni hatari sana kwa miili yetu. Uwezo huo humepekea mwili kukabilina na magonjwa mbalimbali hata ugonjwa wa homa ya mafua ya nguruwe.

Kama huwezi kupata tunda la Komamanga sokoni, basi unaweza kutumia juisi ya komamanga na daima tutunze afya zetu!


Utafiti mpya uliofanywa kwa majaribio umegundua kuwa katika mbegu za nyanya kuna mada asilia,

inayoweza kusadia mzungumzo wa kawaida wa damu na kuzuia damu isigande.


Mada hiyo iliyoko kwenye mbegu za nyanya iligunduliwa mwaka 1999 na Profesa Adim Dutta-Roy.

Jeli hiyo inayozunguka mbegu za nyanya, hunaweza kusaidia mzunguko wa damu.

Jeli hiyo isiyokuwa na rangi wala ladha, huzuia chembe za damu aina ya platelets zisishikane,

suala ambalo hupunguza uwezekano wa damu kuganda, kama inavyofanya aspirini lakini bila kuwa

na madhara.Wachunguzi wa Uingereza wamesema kwamba, athari za geli hiyo huanza masaa matatu tangu

inapoanza kutumiwa na kudumu kwa masaa 18, hivyo inahitaji kutumiwa kila siku.


Wataalamu hao wamependekeza kwamba, kuongeza jeli hiyo katika vyakula mbalimbali kunaweza

kuepusha matumizi ya aspirini kwa ajili ya kuzuia hatari ya magonjwa ya mishipa ya moyo.
 
Asante, ila ndiyo kg 1 sh 20,000
Komamanga kg 1 sh 20,000 si chochote ukiwa nazo kwani utakapo patwa na ahyo Maradhi ya Saratani ya Matiti Aka (Breast Cancer) zitakutoka mara hizo sh 20,000 Mara 20,000 na hutoweza kupona na siku hizi Serikali ilivyozuia kwenda kutibiwa nchini india . Kifo kitakuhus ukipatwa na ahyo maradhi ya Saratani ya Matiti. Afya Bora kuliko Pesa. Pesa inatafutwa na kazi ya pesa ukiwa nayo ni matumizi je afya yako unaweza kuipata wapi?Afya yako ya mwili unaweza kuinunuwa dukani au Hospitali?
 
Back
Top Bottom