Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Inasemekena alikuwa anafuata nyayo za kina Seif Shari Hamadi, na mzee Alhaji Abdu Jumbe... Ni yale yale muendelezo wa Serikali tatu. Lakini kwa bahati mbaya alichelewa sana.Naomba kuuliza, ni kipi kilimsibu Salmin na kampeni yake ya kuongezewa muda kugombea Urais?
Maana naona yeye ni kiongozi wa pili kutoka Zanzibar ambaye aliishia "kudhibiiwa" na CCM!
Naomba kuuliza, ni kipi kilimsibu Salmin na kampeni yake ya kuongezewa muda kugombea Urais?
Maana naona yeye ni kiongozi wa pili kutoka Zanzibar ambaye aliishia "kudhibiiwa" na CCM!
Ubeba ulichopa mipaka, kauli yake zake kuwa "hakuna baba wa taifa wala babu wa taifa" ( Nyerere akiwa hai ) ziliwatia mashaka watu kuwa jamaa akibadili katiba na kuendelea huko mbele hata huo muungano utakuwa matatani.
Mkong'oto aliwapa CUF ikiwa pamoja na kuwasweka ndani takriban miaka 3 viongozi waandamizi wa CUF akiwemo mpwae, mtoto wa dada yake Juma Duni kwa kile kilichoitwa 'uhaini". Ilifika wakati hata dada yake ( mama wa Duni ) alimuomba amwachie akasema muache akae ndani kwa "sio nyanya zile labda zitaoza!".
Nguvu kubwa ya wana mtandao ( Bara ) JK, RA, EL, Membe et al ilisimamisha jaribio la NEC- ZNZ kubadili katiba. Ikumbukwe NEC - ZNZ ilisha ridhia mabadiliko ya katiba.
Wana mtandao (ZnZ ) akiwemo Karume, Seif Khatib, et al kusimama kidete kupinga jaribio la kubadili katika.
Ujinga wa Salmin kutojua SMZ inaongozwa na serikali ya Muungano.
I do like the way u spin Junius. Lakini kwa nini hutaki kueleza ukweli jinsi gani CUF waliiba kura katika uchaguzi huo wa kina Salmin. Kina Salmin walitonywa njama na mikakati ya CUF ya kuuiba kura (na intelligence) wakapuuza wakizubaishwa na vigelele vya katika kiriri. Matokeo yake ni uchafuzi katika uchaguzi ule, but on part of CUF na siyo kina Salmin ambao walikuwa na matumaini. Junius kuwa na courage ya kueleza ukweli.Komandoo alikuwa ni miongoni mwa ile "kama huru" akijifichaficha siku hizo, Marehem Mzee I.A.Wakil alishambonyeza "asifanye papara" akajamuudhi Nyerere, naye komandoo alifuata ushauri wa wakubwa na kuisaliti "kama huru". Hata hivyo bado alikuwa both "mpenda nchi" na "tumbo lake". Madaraka matamu lakini yana mwisho, mwaka 1995 alibwagwa katika uchaguzi mkuu wa vyama vingi na Maalim Seif, komandoo , kama Mzee Mugabe, alishakubali matokeo, lakini unajua tena wapambe nuksi, amri ikatoka kule machinjioni (dodoma), katika kile kilichoitwa kwa siri "do any thing to save the union from anemies", matokeo yakabadilishwa, machinjioni (dodoma)?
.
Na wanamtandao wasingeweza kupenya , bila ya nguvu ya marehemu Diria (Mungu Amlaze mahala pema). Ambaye aliwabeba "Wanamtandao" na kuwapenyeza huko Zenj kwa kutumia mgongo wa uwana-Mapinduzi.Junius,Pakacha,
..waliomshughulikia Komandoo na Dr.Bilali Dodoma ni wanamtandao.
..Komandoo alisaidia kushawishi wajumbe wa ZNZ kumpa kura Mkapa na kumkosesha Uraisi JK mwaka 95 ktk mkutano mkuu wa CCM.
Wakuu kwa anaejua:
Kwa nini Kikwete aliposhinda 1995 uchaguzi ukarudiwa kwa madai kuwa hakufikisha zaidi ya 50% ya kura zilizopigwa.Huu utaratibu ulikuwepo/upo kwenye katiba ya CCM au ni zengwe tu la Nyerere&co?
Na ile ya Bilali na Amani karume je?Sheria za CCM ni kuwa mtu kua mgombea wa CCM lazima ashinde kwa zaidi ya 50%(yani majority). Mgombea mmoja asipo pata hizo asilimia zinazo hitajika kuna kua na runoff kati ya wagombea wawili walio pata kura nyingi zaidi. Sasa JK hakupata more than 50% so kukawa kuna runoff(round ya pili) kati ya yeye na bwana Mkapa. Kwenye hiyo roundoff Mkapa akapata asilimia zinazo takiwa. Hicho ni kiashiria kwamba waliokua wana support wagombea wengine baada ya mbio kuwa kati ya JK na Mkapa waka hamia kwa Mkapa. Watu wengine wanavyo dai ni kwamba Nyerere & co wao walikua wanampigia debe Mkapa na kama unavyo jua Mzee wetu alikua very influential. Sidhani kama kulikua na foul play yoyote. Nyerere knew who he wanted & did everything within the party regulations to get his man. Kama kuna mwenye view tofauti sawa ata tueleza.