Pakacha,
Hebu tuwe wakweli kidooooooooogo tu!
Pindipo (nasisitiza tena, Pindipo) zanzibar ufanyike uchaguzi (angalau wa majaribio) halafu uchaguzi huo uwe huru na haki, ufanyike kihakkki lillahi. Vyama vyote visifanye haya maigizo wanayofanya saivi wakiyaita uchaguzi. Niagulie matokeo.
Na ile ya Bilali na Amani karume je?
Pamoja na mengine mengi Salmin pia aliponzwa sana na tamaa zake za kua rais wa Muungano, kiburi na ubabe wake dhidi ya rais Mkapa, vlichangia sana katika kuwaudhi waamuzi ndani ya CC...
No,Mkuu FMES hayo macho ndiyo wajumbe walimtenda huko Dodoma?
MwanaFA1,
"Sheria za CCM ni kuwa mtu kua mgombea wa CCM lazima ashinde kwa zaidi ya 50%(yani majority). Mgombea mmoja asipo pata hizo asilimia zinazo hitajika kuna kua na runoff kati ya wagombea wawili walio pata kura nyingi zaidi"
Sasa sku ile kule machinjioni(dodoma) nilishangaa niliposikia Mw'kiti (Mkapa wakati ule) akimlazimisha kistaarabu na kumtisha tisha Dr. Bilal aondowe jina lake katika kinyan'ganyiro cha urais kwa kisingizio eti kumwachia Karume amalize temu ya pili (utafikiri kaikodi), wakati huku wanaume tulishajitayarisha kupiga rusha roho kuanzia bandarini dsm hadi zenj, sasa hapa ule utaratibu wa demokarasia ya kuchagua na kuchaguliwa ndani ya CCM ulienda wapi siku ile. Na mm najua mpaka hapo unapojuwa ww kuwa "maza" alienda kulialia na kumwaga michozi eti "ooooh watu wameanza kusahau jitihada za marehemu bwana kwa kumpuuza mwanawe"
Sisi wengine kuanzia pale ndo tukabwaga manyanga eti...
Msaada kwenye tuta Mkuu FMES.
Salmin kuendelea na urais ingebidi Baraza la Wawakilishi wabadili katiba ya Zanzibar. CC ya CCM inahusika vipi?
KATIBA YA JAMHURI, 104 ( 1 )
``Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar atachaguliwa na wananchi katika Tanzania Zanzibar kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Zanzibar, na kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi la Zanizibar inayohusu uchaguzi kwa ujumla au uchaguzi wa Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.``
Ahh Dilunga Mwanazuoni mwenzangu, leo unajifanya kusahau kuwa Katiba ya Tanzania na ya Zanzibar zinafuata amri ya CCM?
CCM wakiamua jambo, ndipo hubadili Katiba ifanye kazi kwa matakwa yao.
Sasa hili la Zanzibar linakushangaza vipi?
Umesahau ni CCM iliyoridhia kwanza kuwa na Vyama vingi ndipo Katiba ikabadilishwa?
Labda nikusaidie kwa mara ya mwisho, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi hupitishwa kuwa Wagombea na kuchujwa na nani kabla ya kwenda kwa Wananchi kupigiwa kura? Jibu ni kwanza Kamati Kuu ya CCM, kabla ya kwenda NEC na hata Mkutano Mkuu wa Taifa!
CC ya CCM ndio nguvu ya nchi na si chombo kingine ati!
mkapa hakutoka nje kwani ndiye aliyeongoza kikao cha kumuondoa jamaa katika tamaa zake hizooo..- political miscalculations, yeye alikuwa ana bank on mkapa, kwmaba kwa sababu alimsaidia mwalimu, kumpa urais mkapa over kikwete basi mkapa hana ubavu wa kumzuia kuwa rais tena wa term tatu,
- wafadhili wasingekubali huu ujuha, ccm siku zote wako careful kuwa on line na wafadhili, ndio maana siku ya kumfundisha adabu salmin kule cc dodoma, salmin aliitwa mbele ya kikao na cc wakamuomba mkapa atoke nje, ili wamshughulikie wenyewe, na kwa hasira ya wajumbe wengi dhidi ya salmin, wakamwambia wazi kwamba hata mgombea wake bilali wanamtwanga na kumpa karume, aliyeshindwa naye!
Respect.
fmes!
mkapa hakutoka nje kwani ndiye aliyeongoza kikao cha kumuondoa jamaa katika tamaa zake hizooo..
Wajumbe wengi walishangazwa na ujasiri wa mkiti (bwm) katika kushughulikia jambo zito kama lile kwa diplomasia ya halii ya juu..na kikao kikisonga na maamuzi safiii wakafikiaaa..
Bwm alimaliza kazi kilainiii sanaa...jamaa ana ujasiri wa uongoziiii
Tusisahau kuwa kiboko ya CUF alikuwa si mwingine bali KAMANDOOO
hilo CCM wanalijua
vile vile tusisahau kuwa CUF na CCM have one thing in common:
wote hawaupendi muungano...the only question nani atakuwa na guts za kusema hilo wazi wazi