Kombe jipya la ligi ya NBC kutambulishwa Juni 7, 2023

Kombe jipya la ligi ya NBC kutambulishwa Juni 7, 2023

Franky Samuel

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2018
Posts
5,195
Reaction score
13,785
BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inawataarifu kuwa kwa kushirikiana na Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Tanzania, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), tutatambulisha Kikombe kipya cha Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC, kesho Jumatano Juni 7, 2023.

Tukio hilo litafanyika mbele ya Wanahabari kwenye ukumbi wa makao makuu ya NBC uliopo Posta ya zamani, Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi.

Baada ya kupokea maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa mira wa miguu kuhusu muonekano wa Kikombe kilichotangazwa msimu uliopita, iliamuliwa kwa pamoja kufanya maboresho katika eneo hilo muhimu ili kuendana na hadhi na kiwango cha Ligi yetu inayoendelea kujizolea umaarufu na mvuto kila siku barani Afrika na duniani.

Wanahabari wote mnakaribishwa kushuhudia utambulisho wa Kikombe hicho ambacho kitakabidhiwa kwa Bingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2022/2023, klabu ya Young Africans Juni 9, 2023 baada ya kumalizika kwa mchezo namba 233 kati ya Tanzania Prisons a mabingwa hao kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Bodi ya Ligi kwa niaba ya TFF na NBC inawashukuru wadau wote wa mpira wa miguu kwa kuendelea kutoa ushauri na maoni chanya kwa lengo la kuboresha zaidi Ligi hi inayoshikilia nafasi ya tano kwa bora barani Afrika kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS).

20230606_220147.jpg
 
 
Ule uzi tuliokuwa tunajadili timu kuchukua kombe moja kwa moja uko wapi? Nilikuwa nawaambia mashindano na ligi zinatofautiana, kuna mashindano kila msimu wanatoa kombe, kuna mengine ili ukae nalo moja kwa moja inabidi ushinde mara 3 mfululizo.
 
Lile kombe la msimu uliopita lilinifikirisha sana utimamu wa akili za viongozi wetu. Lile kombe huangalii mara mbili unaona ni baya,lakini wenye dhamana wao waliona ndio ubunifu mzuri.
 
Wapewe hilohilo boliti la mwaka jana🤣🤣🤣 wanaendana nalo.
 
Afadhali maana wanathiimba walitusema sana Mara jagu, mara kinu, mara mashine ya kusagia mahindi yaani
 
Back
Top Bottom