Kombe la bonde la mto nile

Kombe la bonde la mto nile

Kilakshari

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2008
Posts
350
Reaction score
20
Timu yetu ya Taifa inaanza kampeni za kutwaa kombe la bonde la mto Nile kwa kutupa karata yake ya kwanza kesho kwa kupambana na timu ya taifa ya Misri. Stars ambayo kwa mara ya mwisho ilifungwa bao 5-1 na Misri imesema imejipanga si tu kulipa kisasi dhidi ya Misri bali pia kuhakikisha inashinda kila mechi katika mashindano hayo ambayo Uganda, Kenya, Sudan, DRC na Burundi zinashiriki pia. Kwa upoande wa Misri, imesema inazihofia DRC, Sudan na Uganda katika michuano hayo. Na kamwe Tanzania aiinyimi usingizi. Kwa mtazamo wangu mie japo si vema sana kuyapuuza mawazo ya mafarao hayo lakini Taifa stars ya sasa imebadilika kwa kiasi fulani hasa kwa kupata kipa, walinzi na kocha ambao wanaweza kucheza katika kiwango bora zaidi ya ile ya awali. Taifa stars ya sasa hivi ina uzoefu mzuri kwani imeshacheza na timu za kombe la dunia; Brazil na Algeria. Kwa mtazamo wangu mie Stars piga ua, lazima itapata matokeo mazuri zaidi ya yale yaliyopatikana chini ya Maximo ikiwa pamoja na uwezo wa kushinda mechi hiyo. Ingawa sio kipimo 100%, sisiti kusema kuwa Egypy waliwahi tandikwa na Algeria bao 3 uwanja ule ule ambao hao Algeria ilibidi wafanye juhudi kupata sare dhidi ya Stars. Naamini stars wakigangamala ushindi upo.
 
jamani kuna aliyepata link inayoonyesha game la stars isio na kwikwi naona yangu hapa inagoma kila mara, msaada tafadhali
 
Mzizi wa mashindano haya ni nini? seems to me Wamisri wanataka wawaweke sawa ngozi nyeusi kuhusu Nile na ujumbe upo wazi.

BTW, Stars isitegemee kushinda hapo maana Wamisri wanajulikana for unsportsmanlike behaviour.
 
Tayari kamoja ..upuzi mtupu..ngoja niendelee kufanya mambo mengine ya maana..
 
mh wanacheza kama wapo mazoezini jamani hii timu yetu vipi?
 
Tunaonekana tumechoka mnoooo, msikilize comentator wa kiarabu anakupa haluaaaaaaa haluaaaaaaaaa
 
timu haina ushirikiano kabisa...kipa wa egypt hajadaka hata mara moja
 
Back
Top Bottom