Kombe la buree kwa vituo vya TVna Radio vya Afrika

Kombe la buree kwa vituo vya TVna Radio vya Afrika

fiksiman

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2008
Posts
402
Reaction score
107
Ndugu wa pale Tandale kwa Mtogore, manzese kwa mfuga mbwa na kwingineko ambako huduma ya luninga inapatikana kwa jumuiya na pengne mnajiuliza kombe la dunia kule bondeni itauwaje....msihofu, FIFA inaanda mpang maalum utakao ziwezesha vitu vya televisheni na radio vya afrika kurusha matangazo moja kwa moja bureee kabisa.

Mpango huo utaviwezesha vituo vyote vya umma na binafsi kurusha matangazo kwa ujira wa kugawana pesa za matangazo ya biashara na Chama hicho (FIFA) ilimradi kituo kithibitishe uwezo wa kurusha matangazo hayo bila ubabaishaji. Ila vituo vya kulipia kama dstv,gtv na vingine vya aina hii vitalazimika kulipia kama kawaida.

Harahara jirani msingie tamaa ya kututoza vijisenti....chonde chonde!
 
Last edited:
Back
Top Bottom