Assalam Aleikum, habari yako Mzee wangu naomba kujua ufahamu wako juu ya muundo mzima wa mchezo wa mpira wa miguu kama chombo cha kuongoza jamii Yani social construct.
Hili swala la kuunda michezo limeanza enzi na enzi mfano enzi za falme za kiromania kulikua na gladiator games mfano kama series ya Spartacus au movie The gladiator (Russel Crowe). Ilikua inawaunganisha watu na kuwashaulisha ku rebel. Kuna wataalamu wanafananisha NFL na gladiator games.
Binafsi naamini michezo kama NFL, Basketball, Football, na maonesho mengi kama big brother, miziki inatumika ku 'dumb down' jamii na kuleta muunganiko wa ki artificial kusahau malengo hatimae kupoteza consciousness.
Mara kadhaa vyombo hivi vya kurubuni jamii hutumika purposefully kuhadaa watu kwa epiphany ya muda mfupi na kusahau kabisa azma zao na kujikwamua kifikra.
Upande wa pili pia nafikiri ni biashara haramu ya ku bet iko nyuma ya pazia na matokeo kupangwa kunufaisha watu fulani nyuma ya pazia, watu wanasema kusrma ni conspiracy lakn wahenga walisema lisemwalo lipo, Ahsante.