Kombe la FA msimu huu halipo?

Kombe la FA msimu huu halipo?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Wakati tumeingia duru la pili la msimu wa NBC mpaka sasa sijasikia mechi zozote zikipangwa au kuchezwa za FA Cup.

Ni kwamba msimu huu kombe halipo au kuna changamoto? Kama wana uhaba wa pesa au CRDB wanazingua waniambie tajiri niongeze mzigo. Msimu huu Simba hatutaki kuacha kitu mezani.

NYONGEZA (HAIHUSIANI NA MADA): Zamani mwenyeji wa mashindano huwa hachezi mechi za kufuzu, siku hizi mashindano mengi ya CAF kama AFCON, hadi mwenyeji anacheza mechi za kufuzu, ina maana mwenyeji anaweza asifuzu mashindano yanayofanyika katika nchi yake mwenyewe?
 
Huwa unafatilia kweli Mpira, mbona mechi zinachezwa ila kwenye zile Teams za madaraja ya Chini washaanza kukutana wapunguzane kwanza
 
Nashukuru kwa taarifa. Sijasikia mechi zozote toka msimu umeanza.
 
Tatizo la mleta mada akili yake ipo Kwenye mechi za Simba na Yanga tu!,ila hafuatilii mpira!

Ratiba ishatoka Kitambo
Kuna maisha nje ya mpira. Yanga yenyewe siiangalii labda nikijua wanaenda kufungwa.
 
Maisha ni Mpira na Mpira ni maisha mkuu!

GUSA , ACHIA, TWENDE KWA MAKOLO
Mpira unatuepusha na vitendo viovu ila muda wangu hauniruhusu kuangalia mechi ya Mbuni vs Mabatini. Majukumu bwashee.
 
Wakati tumeingia duru la pili la msimu wa NBC mpaka sasa sijasikia mechi zozote zikipangwa au kuchezwa za FA Cup.

Ni kwamba msimu huu kombe halipo au kuna changamoto? Kama wana uhaba wa pesa au CRDB wanazingua waniambie tajiri niongeze mzigo. Msimu huu Simba hatutaki kuacha kitu mezani.

NYONGEZA (HAIHUSIANI NA MADA): Zamani mwenyeji wa mashindano huwa hachezi mechi za kufuzu, siku hizi mashindano mengi ya CAF kama AFCON, hadi mwenyeji anacheza mechi za kufuzu, ina maana mwenyeji anaweza asifuzu mashindano yanayofanyika katika nchi yake mwenyewe?
Shida yako muda mwingi unautumia kuiwazia Yanga tu. Na ndiyo maana huko kwingine hujui kinachoendelea. Ila kwa kukusaidia; ni kwamba mashindano yapo! Na yanaendelea.

Na mpaka sasa timu zimeshapatikana 64, huku moja ya timu ya ligi kuu (Ken Gold) ikiwa imeshatolewa na timu ya ligi daraja la tatu.
 
Ningekuwa naiwazia Yanga kama mnavyodhani basi ningekuwa naangalia hata mechi zake.

Msimu huu sidhani kama nimeangalia mechi za Yanga zinazofika 5 katika mashindano yote. Embu ngoja nihesabu, Tabora, Simba, Al Hilal na nadhani MC Algier ndiyo mechi pekee za Uto nilizoangalia msimu huu. Hapo inakupa picha ya mtu anayeiwazia Yanga muda mwingi?
 
Simba na yanga ndo hazijacheza lkn timu zingine za PL, championship, FL na RCL zimeshacheza
 
Back
Top Bottom