major mkandala
Member
- Mar 6, 2010
- 74
- 2
VIJANA wa jamii ya kifugaji kote nchini, wanapaswa kuungwa mkono katika suala la kuendelezwa kisoka, kwani kwa kufanya hivyo kutawafanya wajitume zaidi na kuacha fikira potofu kuwa wametengwa katika michezo.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Iddi Kipingu wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kuwania Kombe la Lowassa mjini Monduli juzi.
Kipingu alisema kitendo cha Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kuanzisha Kombe hilo ni kutaka kuona vijana wa jamii ya Kimasai wanaachana na hisia kuwa wao hawawezi kucheza soka na badala yake wanapaswa kuchunga mifugo tu.
Alimsifu mbunge huyo kwa uamuzi wake wa kuanzisha timu ya wanawake, kwani ni wilaya ya pili hapa nchini kufanya hivyo ukiachilia mbali Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti huyo alisema vijana wa Monduli katika soka wanaweza kufanya vizuri kwani wana maumbile mazuri kimichezo kama ya watu wa Afrika Magharibi.
''Tunapaswa kumuunga mkono Lowassa kwa kufanya jambo hili, ili Taifa liwe na vijana wenye uwezo wa kisoka na vijana wa kifugaji waweze kujua kuwa taifa bado linawajali,''alisema Kipingu.
Naye Lowassa alisema lengo la kuanzisha Kombe hilo miaka kumi iliyopita ni kutaka kuona vijana wanashiriki vyema michezo na kuacha tabia ya kujiingiza katika mambo yasiyokuwa na maana.
Lowassa alisema mwaka huu zawadi na gharama za mashindano zitatangazwa hapo baadaye.
Mwaka jana mashindano hayo yaligharimu zaidi ya Sh milioni 66, vijana wawili walioonesha uwezo mkubwa katika soka waliteuliwa kwenda kuona Kombe la Dunia litakalofanyika Afrika Kusini kuanzia Juni mwaka huu.
Mbali ya vijana hao, ambao ni Achi Ngomelo na Kayai Alfred, pia Katibu wa Chama cha Soka Wilaya ya Monduli, Ndauka Njelekele naye atakuwa miongoni mwa wanamichezo watakaoenda kushuhudia fainali hizo za Kombe la Dunia .
Katika mashindano ya mwaka huu, timu 25 zitashiriki kuwania Kombe la Lowassa na timu zote zimepewa seti moja ya jezi na mipira miwili.
Katika mchezo wa ufunguzi juzi, timu ya soka ya wanawake ya Kinondoni kama wageni waalikwa iliifunga timu ya wanawake ya Monduli mabao 2-1 katika mchezo wa aina yake uliochezwa Uwanja wa Bomani Monduli.