Kombe la Shirikisho Afrika | CD DE Agosto Vs Namungo FC, Uwanja wa Azam Complex

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kuendelea kutimua vumbi leo February 21, 2021 kwenye uwanja wa Azam Complex, ambapo wenyeji CD De Agosto wanapambana na Namungo FC

===========

Namungo FC wakiwa ugenini kwa mujibu wa kanuni, wametakata vilivyo baada kuiadhibu bila huruma Cd de Agosto mabao sita kwa mawili katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex

Mabao ya Namungo yakifungwa na Manyanya 32' Sabilo 38' 55' akifunga mabao mawili, Lusajo 59, Kwizera 68' na Stephen 71' Sey

Mchezo wa pili utafanyika siku ya Jumatano kwenye uwanja huo huo wa Azam Complex, Namungo FC wakiwa wenyeji ambapo Namungo FC wanahitaji sare tu kutinga makundi kombe la Shirikisho Afrika.

FT: Cd de Agosto 2-6 Namungo FC



 
Mpira umeanza uwanja wa Azam Complex, kombe la Shirikisho Afrika.

13' Cd de Agosto wapo mbele kwa bao moja kufuatia mkwaju wa penalty ambayo ilipanguliwa na ikafungwa tena na Brian Moya

Cd de Agosto 1-0 Namungo FC
 
Yani Namungo wakishindwa kuitumia hii nafasi sitawaelewa kabisa, mechi mbili zote nyumbani kwenu halafu mtolewe?!
 
30' Wanacheza vizuri Namungo FC wakitulia watasawazisha na kuongeza

Cd de Agosto 1-0 Namungo FC
 
Yani Namungo wakishindwa kuitumia hii nafasi sitawaelewa kabisa, mechi mbili zote nyumbani kwenu halafu mtolewe?!
Wakicheza kama walivyokutana na KMC anapigwa nje ndani apo apo azam complex.
 
Sabiloooo Gooooooooooooal, Namungo FC wanaandika bao la pili kupitia kwa Sixtus Sabilo

CD De Agosto 1-2 Namungo FC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…