Kombe la Shirikisho Live: Yanga Afrika vs Etoile du Sahel

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
Kama kawa leo ndio leo, Wote tuiombee Yanga itutoe kimasomaso.

Updates zote ziwekwe hapa!



Mashindano: Kombe la Shirikisho la CAF, Raundi ya 2, Mechi 1

Yanga Afrika vs Etoile Sportive du Sahel

Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Saa 10 Jioni


Updates:

Full Time Yanga 1 - Etoile 1

Dakika ya 40 Yanga 1 - Etoile 1

Yanga 1 - Etoile 1 {Amour Amine}

Half time : Yanga 1 - Etoile 0

Dakika ya 40 : Yanga 1 - Etoile 0 {Cannavaro dk 1}

Dk 47.
Yanga: 1 - 1 ETOILE DU SAHEL
 
Yanga tumieni kikosi hiki ili kuwapiga waarabu leo.
Hiki ndio kikosi kinachotakiwa kuanza leo:
1.Barthez
2.Juma Abdul
3.Oscar Joshua
4.Canavaro
5.Yondani
6.Twite
7.Msuva
8.Niyonzima
9.Tambwe
10.Sherman
11.Ngassa.
Hapa timu itakua inashambulia wakati wote na pande zote na hii itawazuia wao kupanda.
Pia mfumo huu utasaisaidia Yanga kuwa na washambuliaji asili wawili pale mbele(Sherman na Tambwe)Huku Msuva akitokea pembeni na Ngassa ili kuipa nguvu safu ya ushambuliaji.
 
DAKA MTUMBA;

Mkuu ni kweli kwamba kila mtu ana maoni yake ila namba 8 ya Young Africans aliyeiva saa hv na anayeibeba timu ni Telela"Abo Master" angefaa:; huyo Niyonzima arud kuwa winga; shida ya hapo ni kwamba kuna mchezaji atakuwa sacrifised kuwekwa benchi, huu ni mtazamo wangu
 
Last edited by a moderator:
Hivi ni kwanini mechi ya kwanza lazima tuanzie nyumbani na kumalizia ugenini?
MUNGU ibariki Tanzania,
MUNGU ibariki Yanga Africa.
 
Mkuu Plesis ,ni kweli Telela yupo vizuri kwa sasa.But sidhani kama leo atakua fiti kucheza maana siku chache zilizopita nilisikia wanasema Telela ni mgonjwa so anaweza asicheze leo.
Anyway,tuwasubiri wadau wa Yanga waje watuthibitishie kuhusu Telela!
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli hata mimi sijajua kwa nini Yanga michezo yote mitatu wanaanzia nyumbani? Nakumbuka miaka ya nyuma utaratibu ulikuwa unafahamika kabisa kwamba timu ikianzia nyumbani basi ikifanikwa kusonga hatua nyingine basi itaanzia ugenini. Mwenye kujua taratibu za sasa atujuze , inakuwaje michezo mitatu yote timu inaanzia nyumani. Au njama? timu zetu za ukanda wa mashariki zisisonge mbele?
 
Hiyo kuanzia nyumbani ni mipango ya kutubana. Waarabu wana mipango sana. Dawa leo ni kushambulia mwanzo mwisho. Tusiwape pumzi. A goid defence is an offence. Daima mbele nyuma mwiko!
 
Jaman TBC 2 watakuwepo uwanjani kuwaletea mtanange Wa kukata na shoka kati ya miamba ya Tanzania Dar young African, YANGA dhidi ya miamba ya Tunisia Etoile du Salehe kuanzia majira ya sasa kumi kamili jion, hii ni kwamujibu Wa kipindi cha michezo asubuhi TBC2. kwa pamoja twaweza YANGA DAIMA mbele nyuma MWIKO
 

Aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaghhhhhhhh! Hawa Jamaa Wapuuzi Sana Mkuu. Kwanini Hawakusema Tokea Jana? Nimeshajikatia Tayari Tiketi Yangu Ya Buku Gwala. Wamenitia Hasara Kweli Kweli!
 
Aje. Tutampa kazi ya kugawa maji ya kunywa kwa wachezaji wetu.

Manji aliahidi kutumia utajili wake wore kuhakikisha okwi hachezei Simba Mara nitaenda CAF, FIFA..kumbe mlikuwa mnataka aje kugawa maji....lol.....Leo mnapigwa na ninasema mpigwe tu maana mkishinda tutapata shida mtaani..
 
Nilijua hili litakuja tu sema zile zilikuwa mbwembwe za watu kujaa uwanjani na kupandisha kipato cha kuvuna
 

Hapa Ndipo Najiaminisha Umuhimu Wa Elimu Ya BRN Nchini Tanzania. Naomba Kujua Hiyo Timu Ya Etoile Du Salehe Ni Ya Kutoka Kijiji Chako Gani Hapa Duniani? Ninachojua Kuna Timu Iitwayo Etoile Du Sahel ( Nyota Ya Sahel Inayong'aa ). Tuepuke Sana Kuonyesha Udhaifu Wetu Wa Kimantiki Humu Mitandaoni Na Tuache Kukurupuka. Ni Ushauri Tu Lakini!
 
Manji aliahidi kutumia utajili wake wore kuhakikisha okwi hachezei Simba Mara nitaenda CAF, FIFA..kumbe mlikuwa mnataka aje kugawa maji....lol.....Leo mnapigwa na ninasema mpigwe tu maana mkishinda tutapata shida mtaani..

Nyie saizi yenu mgambo, mtasubiri sana.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…