maisha yangu yote nimekuwa nikiishabikia manchester united na barcelona ila kwangu mimi combination iliokuwa ikinivutia zaidi ni kati ya John Terry na Ricardo carvalho.
ila nilikuwa nakerwa zaidi na vyombo vya habari hususani vya kiingereza kumsifia zaidi john terry kuliko ricardo carvalho ambaye ndiye aliyekuwa ni hodari zaidi.
na hata ukijaribu kufuatilia kwa umakini utagundua baada ya ricardo carvalho kuondoka chelsea na kuelekea real madrid ndipo terry naye udhaifu wake ulipoanza kuonekana.
msimu wa 2004/2005 chelsea waliruhusu magoli 15 tu kufungwa na pia mechi 25 walicheza bila ya kuruhusu goli.
kwenye mechi za ugenini chelsea waliruhusu magoli 9 msimu mzima.
msimu wa 2005/2006 chelsea waliruhusu magoli 22
tokea aondoke ricardo carvalho chelsea wameshasajili mabeki kama gary cahill, kurt zouma, david luiz na rudiger lakini hakuna ambaye ameweza kusimama na consistent form kama ilivyokuwa kwa ricardo carvalho, sijui huyu muhuni wa kireno aliyepiga kazi ya kishenzi pale old trafford kwenye 16 bora alipokuwa fc PORTO yuko wapi.
kwangu mimi combination ya carragher na samy hyppia nadhani haikustahili kuwepo kwenye list ya combination bora ya ulinzi ukilinganisha na combination kama vile;
Tony Adams na Steve Bould/Martin Keown (Arsenal)
Frank Leboeuf na Marcel Desailly (Chelsea na ufaransa)
Steve Bruce na Gary Pallister (Manchester United)
Lucas Radebe na Rio Ferdinand (Leeds United)
Sol Campbell and Kolo Toure (Arsenal)
Martin Laursen na Olof Mellberg (Aston Villa)
mauricio pellegrino na roberto ayala (valencia fc na argentina)