FANANI MTENZI
Senior Member
- Jul 4, 2017
- 106
- 95
KOMBORA KIOTANI-41
BONIFACE BIRAGE
TULIPOISHIA
DEDANI ANAOKOLEWA MIKONONI MWA WATEKAJI NA SHUNIE ANAPELEKWA SEHEMU YA SIRI NA AFISA HUYO WA USALAMA.HUKO DEDANI ANAMWAMBIA UKWELI SHUNIE KWAMBA AMEMSHAMBULIA MTU ANAITWA TWALIPO NA SASA ANASAKWA NA POLISI.SHUNIE ANAAHIIDI KUMTETEA DEDANI.UPANDE WA PILI VIDEO YENYE USHAHIDI KUWA MUME WA RAIS KILUA AMEUA MTU INAFIKA IKULU NAKUANGUKIA MIKONO YA CHIFU WA IKULU BWANA SERAMBOVU AMBAYE ANA DHAMIRIA KUITUMIA VIDEO HIYO KAMA WEMBE WA KUMCHAFUA RAIS KILUA.
JE.ATAFANIKIWA?
HUU NI KAMA MSIMU MPYA WA MWENDELEZO WA RIWAYA KOMBORA KIOTANI
…
Ushahidi ulioangukia mikononi mwa Serambovu ulikuwa tosha kumpa kiburi cha kumdhibiti Dedani na hakika asingefanya lolote mbele yake ikiwa yeye Serambovu anamiliki ushahidi mkubwa wa mauaji yaliyotekelezwa na mume wa rais Kilua.Hili lingekuwa pigo linguine kubwa sana kwa familia ya rais Kilua ambalo lingemsambaratisha.Serambovu alitabasamu vizuri sana kuona neema ya kibabe imeangukia upande wake kwa mara nyingine tena na sasa yeye ndo mcheza karat azote.
Serambovu alikwisha agana na polisi aliyemletea ushahidi ule.Kisha alichukua simu yake na kupiga namba Fulani akaweka simu masikioni.Simu iliita kwa muda huku akisubiri kwa shauku kubw.Alikuwa hatua nzuri kwa mipango yake.
“Ndiyo chifu unaendeleaje?”
“Kwema mkuu.Nimepata jambo jema nahakika litakuwa mwiba kwa madam president safari hii lazima abwage manyanga.”
“Jambo gani hilo?”
“Ninao ushahidi ukionesha akishiriki mauaji.”
“Ushahidi gani?”
“Kuna mtu anaitwa Twalipo ndo ameuawa na mume wa rais.”alisema Serambovu.
“Very good.”sauti ya upande wa pili iliitikia kwa ukavu.Serambovu akatabasamu nakufurahia kwa jambo hilo akijua sasa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Mambo yalianza kuiva katika uandaaji wa mipango yake.Serambovu alifungua droo nakutoa picha yake akiwa na rais Kilua katika moja ya makongamano makubwa.Alijuafika wanatakiwa kuwa pamoja lakini sio Dedani awepo.Kilua alikuwa mali yake.Amethibitisha hilo mara kadhaa na hata kufikia hatua yakujiona yeye mungu mtu kwa Kilua.Kila nyakati alikuwepo hata alipopewa madaraka ghafla bado alikuwepo yeye kwa wakati ule akisimama upande wake.
“You are mine alone and we shall keep this power together.”alijisemea Serambovu.Akiwa pale alishangaa kuona Kilua akiingia ghafla ofisini kwake.
Serambovu akainuka akimtizama.
“Shani ni mwanao.”alisema Rais Kilua akimwangalia SErambovu usoni kwa umakini wa hali ya juu.
Serambovu akashtuka sana.Hii ni mara ya pili Kilua anarudia msemo huu ila tofauti kwa sasa ni tofauti na kipindi kile.Wakati ule ilikuwa kama fumbo na sasa ni waziwazi ana mwambia usoni.Serambovu aliratibu mipango ya kutekwa kwa Dedani na mwanae akijua anamkomoa kumbe anaikomoa damu yake.
“Chochote unachokifanya mfikirie huyo mtoto.”ulikuwa ujumbe mzito sana kwa yeye kuupokea na hakutegemea kabiisa kama ingetokea kwa jambo kama hilo.Japo alihisi nakukiri kuna uwezekano wa Shani kuwa mwanae lakini hakuwa na uhakika asilimia mia moja.Kilua alikuwa amemuweka mumewe kiganjani pamoja nakushiriki kuihujumu ndoa yake lakini Serambovu hakuwana uhakika kama kweli Shani anaweza kuwa mwanae.Alijua kwa vyovyote Kilua alikuwa anamrubuni mumewe lakini angezaa naye kwa namna moja au nyingine.
Serambovu alisogea akamkumbatia Kilua.
“Najua mimi nawewe tunashea damu.Nilihisi lakini sikuwa na uhakika kama kweli mtoto huyu ni wa kwangu.Nakuahidi kushirikiana nanyi katika kumrudisha mikononi mwetu.”
“Ila naomba jambo moja kutoka kwako.”alisema Kilua akijitoa mwilini mwa Serambovu.
“Anything for you madam president.”alisisitiza Serambovu akijiamini.
“Don’t tell Dedan anything.”alisema Kilua.
“Anapaswa ajue.”
“Nyinyi wote mna nafasi katika maisha yangu.Wewe ulikuwa mwanaume wangu wa kwanza.The greatest love of my life.The first of my youth and womanhood.Young mighty love in the sun.”alisema Kilua akisisitiza maneno yake.
Kisha Serambovu akauliza,”Vipi kuhusu huyo bwege aliyeshindwa kukupa hata mimba.Kazi kulea watoto wa watu.”
“Usimdharau.Yeye ndo wa mwisho kwangu.Ndo mume wangu ndo mwanaume wa kuishi naye and I know I have found reasons to love him more.He won’t betray me.”alisema Kilua akijiamini.
Serambovu alifikiri kidogo kisha akasema<”Sawa madam president tutaona.Asante kwa kunizalia mwana.”
Kilua hakusema kitu kuna wakati alijutia jambo hilo.Lakini ilikwisha tokea.Na sasa anaujauzito mwingine wa Serambovu.Kumbe wakati wanaongea maneno yale tayari Dedani alikwishafika ikulu na Shunie na walikuwa wanaelekea ofisini kwa Serambovu.Dedani alifungua mlango bila hodi nakuwafanya watu hawa washtuke sana.Kisha Dedani alienda hadi ilipomeza ya Serambovu akachukua kidude Fulani cha kurekodia sauti kisha akakiwasha.Lilikuwa tukio la ghafla sana kiasi cha kumfanya Kilua na Serambovu watetemeke.Shunie alikuwa kasimama nyuma ya Serambovu.Leo patachimbika hapa!
Kilua aliwahi nakukishika kidude kile kisha akakitupa chini nakukikanyaga nakukikvunjavunja.Serambovu roho kidogo imsimame.Kuwahi kwa rais Kilua ilikuwa pona yake.Kitendo cha Dedani kuingia ghafla nakuelekea moja kwa moja kwenye meza kisha akachomoa kifaa hicho kwa lengo lakusikiliza hayo mazungumzo ni dhahiri alikuwa ameweka huo mtego kwa mida mrefu sana na siajabu kuna mengi ameshayasikia lakini inakuwaje aweze achilia mbali wazo la kutegesha mtego hulo?
“Mme wangu ni nini unafanya sasa?”aliuliza Kilua.
“You can’t stop me!”alisema Dedan kwa hasira.
“Kunitegeshea vinasa sauti faida yake nini?”
“Shida yangu ni huyu afriti nambari moja!”alisema Dedani akisahau kama mwanamke huyu ni rais.
“Ananifanyia ushushushu mimi?”Serambovu akainguilia kati kwa jazba maana alijiuliza maswali kadhaa Dedani alitumia muda gani kuwasikiliza na je ni kweli anajua walichozungumza au amekuja akahisi rais Kilua atakuwepo ofisini kwa Serambovu.
Kilua alimshika Dedani mkono nakumuondoa pale kwa haraka sana wakaelea eneo linguine la ikulu.Kilua alipiga hatua kadhaa na moja kwa moja alimpeleka chumbani kwake kisha akaufunga mlango..
“We need to talk.”alisema Kilua akimwangalia mume wake huku moyo ukimuenda mbio mfululizo.
Dedani aliketi kwenye sofa pembeni.Walikwisha wasili ikulu wakiwa na Shunie ambaye sasa alihisi wivu mkubwa kila akimuona Dedani karibu na Kilua.
“No more lies nataka nijue ulikuwa unafanya nini ofisini kwa Serambovu?”
Kilua alisogea kwenye sofa lile akaweka mkono wake mmoja kwenye kifua cha Dedani.
“Mimi rais wa taif hili na makazi yangu ni ikulu ninaweza kuingia popote kwa muda wowote ule.”
“Hata kama lakini sio kwa uhuru huu?Serambovu ni hatari kwa mke wangu!”alisema Dedani kwa jazba.
“Unataka kuujua ukweli?”aliuliza rais Kilua.Kitu alichotaka kukisema kwa miaka mingi ilifika muda alitakiwa kukisema.Kitendo cha kugundua mumewe amekuwa akiweka vinasa sauti kilimtisha na ile kukuta kwamba anaweza kuja kushtukiwa siku moja na ikawa fedheha alihisi ni mwiba mkubwa sana.Aliona bora aivujishe siri ile mwenyewe kuondoa mzizi wa fitina.Lakini alitaka iwe maalum pengine angemchukua Dedani nakuandaa mlo jioni maalum kama familia ili aweze kuchuja nakupembua siri zote kwamba amekuwa akimla mgongo siku hadi siku.
“Mke wangu ni bora tukawekana wazi maisha yakuhisiana ubaya hayana mema.Mimi sipendi kuishi kwa mashaka nimechoka sana mama watoto ingekuwa vyema tuwekane sawa.Kwanini Serambovu ana sauti sana kwenye maisha yako?Ukimuondoa utapungukiwa na jambo gani?”
Kilua alifikiri akapiga picha nakuona ni jinsi gani Dedani atachukulia jambo hilo?Aliona kama Dedani akiwa amepanda na jazba nap engine kumletea fujo!
“Kwa muda mrefu nimekuwa na mahusiano ya kimapenzi na Serambovu.Nilidhani ningeacha lakini imekuwa tatizo kwangu nakujikuta nikiendelea kukusaliti mara kwa mara hali ambayo ni mbaya.Kibaya zaidi..”alisita kusema.
Dedani alihisi mwili wote ukifa ganzi.Yale maneno aliyoambiwa bwana Kavu kuwaa Serambovu analalia kifua cha mkewe ni ukweli mtupu na sasa amethibitisha mkewe mwenyewe.
Dedani akajikaza kisabuni.Aliutaka ukweli na sasa anaenda kuusikia nakujifunza namna ya kuishi nao.
“Sema.”
“Nilipata mimba…”kigugumizi kikamshika mama Shani kisha akaendelea,”Shani si mwanao.Ni mtoto wa Serambovu.”alisema rais kiLUA akimwambia Dedani aliyehisi sofa lile lina misumari.Picha ilimjia kichwani siku alipoambiwa mkewe ni mjamzito.Anakumbuka alivyojitahidi kumlea mkewe akiwa mjamzito.alinunua vitabu vingi akijifunza namna ya kumtunza mama kijacho wake halafu leo anaambiwa huyo mtoto si wakwake?Anakumbuka tarehe ya mtoto kuzaliwa na kilio cha kwanza cha Shani!Alikumbuka vyote DEDANI alikumbuka hadi alipombeba Shani nakumlea tena alionesha upendo mkubwa sana kwa binti yake huyo kuliko maelezo.Halafu mama wa mtoto anasema si wa kwake?
“Noo!”alisema Dedani akiwa amechanganyikiwa.
“She is your daughter legally but biologically Shani is not your blood.!”alisema Kilua akihuzunika.Lililkuwa jambo zito sana kulitamka.
“Muongo!Muongo!Muongoo!She is my daughter!Shani ni wangu peke yangu!”alisema Dedani machozi yakimtoka mfululizo.Ulikuwa mwiba mkubwa sana kwenye maisha yangu.Alikumbuka kalivyokuwa kadogo tena kachanga akikabeba hadi alipokuwa mkubwa.Mawimbi ya upendo kwa mtoto wake wa kike yalikuwa yenye nguvu bila kutikiswa na leo anaambiwa huyu mtoto si wa kwake?Amempa hadi jina lake lakini leo hii anaambiwa sio damu yake?Alitekwa naye nakujitahidi kufanya kila awezalo lakini leo aanaambiwa ni mtoto wa adui yake nambari moja?
“Tasha na John pia sio wa kwako!”KIlua akazidi kueleza zaidi.Hao ni wadogo zake Shani.Kilua aliwaficha mbali baada ya kuona familia yake inafuatiliwa.
Dedani akamshika mkewe shingo akitaka kuikunja kwa nguvu.Walinzi walikuwa nje wasingeona walijua tu rais Kilua alihitaji faragha na mume.
“Hata sasa nina ujauzito wa Serambovu.”alisema Kilua.
Dedani alitumbua macho,”Ina maana mtoto wa kwanza ni wa nje?”
“Ndiyo.”
“Wa pili nje?”
“Ndiyo.”
“Watatu nje|?”
“Ndiyo.”
“Na hiyo mimba ni ya nje?”
Kilua alitikisa kichwa.Dedani alijikuta akimuachia shingo nakumtwanga ngumi ya tumbo paa!Ilikuwa na hasira tu.
:”Utaniua mme wangu!”alipiga kelele KILUA nakufanya walinzi wafungue mlango nakuingia kwa haraka.Wakamkuta Kilua ameshika tumbo akigaragara!Walinzi walimuwahi rais maana alikuwa na hali mbaya!Dedani alikuwa amemjeruhi mkewe tumboni na mbaya zaidi alikuwa mjamzito hazikupita dakika mbili Kilua alianza kuvuja damu!
“Mwite daktarii!”alisema moja ya walinzi.
“Alert all units red code!”walinzi walianza kupashana habari.Hali ya mkuu ilikuwa mbaya.Kilua aliondolewa chumbani kwake nakupelekwa kwenye hospitali ya ikulu ikiwa na kila kitu madaktari walimpokea maana huwa tayari muda wote endapo itatokea dharula.Habari ile ilifanywa kimyakimya isijulikane.
Walinzi walimkamata Dedani!