Komredi Kachebonaho atoa futari kwa Kaya 300 Kyerwa

Komredi Kachebonaho atoa futari kwa Kaya 300 Kyerwa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

Komredi KACHEBONAHO Atoa Futari kwa Kaya 300 Kyerwa

Mjumbe wa Baraza kuu la jumuiya ya vijana UVCCM Taifa kutoka mkoa wa Kagera Ndg. Leodigar Kachebonaho ametoa mkono wa Futari kwa kaya Zaidi ya 500 zenye uhitaji wilayani Kyerwa Mkoani Kagera.

Mbaraza huyo amefanya tukio hilo Aprili 06, Mwaka huu ukiwa ni mwendelezo wa kila mwaka kuwafuturisha waislamu hasa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.

Akiongea mara baada ya kugawa Futari hiyo LEODGER LEONARD KACHEBONAHO amesema kuwa katika kipindi hiki Cha mwezi mtukufu wa Ramadhan ni kipindi ambacho waislamu kote nchini wanakitumia kuliombea Taifa na viongozi wake hasa Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan hivyo wanatakiwa kupongezwa na kushukuriwa.

Amesema kuwa Futari hiyo aliyoitoa ni katika kile alichojaaliwa na Mwenyezi Mungu hivyo amewaomba waumini kukipokea na kuendelea kumuombea.

Sambmaba na hayo amewaomba waumini na viongozi wa dini kuendelea kuhubiri Amani upendo na mshikamano ili kuweza kuleta Taifa lenye watu wanaomuogopa Mungu kwa kila wanalolitenda.

Kwa upande wake Sheikh wa wilaya ya Kyerwa Sheikh Nouh Badru Mlashani amemshukuru Mbaraza huyo kwa kuwa na moyo wa kukumbuka nyumbani na hasa kuwakumbuka waislamu waliofunga licha ya kwamba yeye siyo Muislam.

Amesema vijana wengi wenye uwezo wamekuwa wakishindwa kutoa hata sadaka kidogo kuwapa wenye uhitaji na kuongeza kuwa Kachebonaho amekuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa vijana ambao wanayomafanikio kuwasaidia watu wenye uhitaji.

Ameongeza kuwa Futari hii aliyoitoa kwa kaya 500 kutoka misikiti Saba ya wilaya ya Kyerwa ambapo kila kaya ilipata kilo tano za mchele imeleta tabasamu kwa waislamu ambao kwa namna Moja ama nyingine hawakuwa na uhakika wa kupata futari huku baadhi ya waumini waliopokea Futari hiyo wakimshukuru Mbaraza na kumuonbea Kwa Mungu aendelee kumfungulia milango ya Kheri.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-04-07 at 15.30.42.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-07 at 15.30.42.jpeg
    44.3 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-04-07 at 15.30.43.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-07 at 15.30.43.jpeg
    52.7 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-04-07 at 15.30.44.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-07 at 15.30.44.jpeg
    61.4 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-04-07 at 15.30.44(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-07 at 15.30.44(1).jpeg
    45.3 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-04-07 at 15.30.45.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-07 at 15.30.45.jpeg
    46.8 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2024-04-07 at 15.30.45(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-07 at 15.30.45(1).jpeg
    48.9 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-04-07 at 15.30.46.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-07 at 15.30.46.jpeg
    49.3 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-04-07 at 15.30.46(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-07 at 15.30.46(1).jpeg
    51.3 KB · Views: 6
Back
Top Bottom