Bahati mbaya sana mzee Kinana hakuweza kujiba hoja yoyote zaidi ya kurudia yanayofahamika, na kuleta kauli zenye utata zinazoibua maswali mengine mengi. Kutoka kwenye kauli zake zenye utata, ametengeneza ajenda za watu kumwonesha ama asivyojua au alivyojitoa ufahamu kwaajili ya kutetea mambo ambayo hayapo sawa.
Majibu atakayopewa sasa, atajilaumu kwa nini alisema aliyoyasema.
Hoja za msingi:
1) Katiba yetu ni mbovu, na hilo linafahamika kwa miaka mingi. Wananchi walikwishamaliza kutoa maoni yao kupitia tume yenye weledi ya Warioba. Kuunda vitume vingine visivyoeleweka ni ujinga na uhayawani wa hali ya juu, na ni mbinu chafu za kuchelewesha wananchi wanachokitaka. Tume ya Jaji Warioba ilifanya kazi kubwa sana ikichukua sample population kubwa sana.
2) Tunahitaji tume huru ya uchaguzi, siyo tume kiinimacho. Haiwezekani Rais watu wanaopendekeza majina ya viongpzi wa Tume yatoke kwa watu ambao ni wateule wa Rais. Kama Rais ndiye atakayefanya uteuzi wa mwisho, ni lazima wanaopendekeza majina wawe ni. Watu huru ambao hawapo kwenye mongwa la Rais. Yaliyofanyika ni usanii na kuwafanya Watanzania ni wajinga.
3) Muungano wa watu wawili hauwezi kuendelea kuwa muungano kama walioungana, mmoja anaishi na mwingine ameuawa. Bunge la mwaka 1993 liliazimia kuwe na Serikali 3. Kupitia tume ya Warioba wananchi wakasema wanataka serikali 3. Ninyi akina Kinana ni viziwi au wanafiki kiasi cha kutotambua matakwa ya umma wala kujua mantiki ya kuungana? Wananchi tuongeze moto wa kutaka muundo mzuri wa Muungano, mpaka hawa waziba masikio wasikie.
4) Haiwezekani Tanganyika iuawe, Zanzibar iishi, halafu Wazanzibari ambao kwao Mtanganyika haruhusiwi kumiliki hata robo ekari, wawe wanagawa hovyo rasilimali za Tanganyika. Ugawaji wa bandari za Tanganyika, mbuga za wanyama na hifadhi za misitu kwa Waarabu, ni ubatili na ushetani wa hali ya jui dhidi ya Watanganyika.